Alhamisi, 2 Juni 2016

KAIMU KATIBU MKUU NDUGU SHAKA HAMDU SHAKA AHUDHURIA MSIBA WA LUTENI YAREDI

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akiwa na  Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Emanuel Nchimbi.

 
 
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka(MNEC)  ameongoza ujumbe wa UVCCM katika mazishi ya Lt Mstaafu Joseph Yeredi. Mjumbe wa Halmashauli Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza 2012-2017 na Mwenyeikti Mstaafu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza/ Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa 2003 -2008.
Ujumbe huo umejumuisha baadhi ya Wenyeviti wa Mikoa UVCCM , wilaya UVCCM, wajumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa, watendaji wa ngazi za mikoa na wilaya pamoja na maafisa wa UVCCM makao Makuu. Mazishi ya Lt Yaredi yamefanyika Kijijini kwao Kalebezo Jimbo la Buchosa, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza.
Katika uhai wake Marehemu Lt Yaredi akiwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji alitumia vyema nafasi yake kusimamia na kutetea haki na maendeleo ya UVCCM hasa katika masuala ya kuimarisha uchumi ndani ya jumuiya. Akitoa Salamu za rambirambi kwa niaba ya Umoja wa Vijana wa CCM , Katibu Mkuu amesema kiongozi huyo kilichokufa ni kiwiliwili chake bali fikra zake, mema aliyokuwa ameyafanya katika uhai wake yatabaki kuwa alama isiofutika.
Shaka amemtaja Marehemu kuwa ni kiongozi wa kuigwa na kupigiwa mfano kwa matendo yake thabit hasa katika maisha ya siasa.
"Wakati leo hii tukiweka mwili wake katika udongo tulioumbiwa nao , jina lake milele litabaki kwenye kumbukumbu zetu na yeye atabaki kuwa alama ya uzalendo, umakini , ujasiri na usikivu uliyojaa busara". Mungu ampokee na kuiweka mahali pema roho ya Marehemu Ameen. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali akiwemo Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ngd Emanuel Nchimbi, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mwenyeikti wa CCM, Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wilaya na viongozi wengine kadhaa.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu