Unordered List


MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA PWANI MOHAMMED NYUNDO AIPONGEZA WIZARA YA ELIMU

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Ndugu Mohammed Nyundo akizungumza na Vijana hawapo pichani.
TAARIFA

 Kwa niaba ya Vijana wa CCM Mkoa wa Pwani, Kwanza kabisa Tunapenda kuipongeza wizara ya Elimu Kwa juhudi mbali Mbali zenye nia thabiti ya kuendeleza sekta ya Elimu Kwa Madhumuni ya kujenga Tanzania imara.
 
Pili, tukiwa kama wadau muhimu Kwa mustakali wa Vijana wa Tanzania, ni vyema kuonyesha Msimamo wetu juu ya masuala mbali mbali, Hususani yanayowahusu Vijana na mustakali wa Maendeleo yao. Tunapenda kusema yafuatayo juu ya kadhia ya Suala la Mgogoro wa Wanafunzi za...idi ya 7000 wa Kozi maalum ya taaluma ya ualimu chuo kikuu Dodoma kama ifuatavyo.
Moja, Wizara ya Elimu iweke bayana juu ya masuala mawili, Suala la Vijana 480 waliodahiliwa kimakosa na kukosa sifa za kujiunga na Elimu ya juu na kupata mikopo ya serikali kama alivyoeleza Mh Rais, na Suala la Vijana zaidi 7000 waliorudishwa nyumbani Kwa sababu za Mgogoro kati ya Uongozi wa chuo, wahadhiri na serikali. Mambo haya yameleta mkanganyiko mkubwa katika jamii ya watanzania na Kwa wasioitakia mema Serikali ya CCM wanapata mwanya wa kupotosha Suala hili.
 
Pili, Mh Waziri wa Elimu amenukuliwa akisema ya kwamba vijana hawa zaidi ya 7000 waliorudishwa nyumbani walidahiliwa kwenye Kozi hii maalum Kwa sababu ufaulu wao ulikuwa wa juu. Hivyo hawana hatia. Wamekuwa Wahanga wa mkanganyiko wa maamuzi ama kutoelewana Kwa vyombo na taasisi vinavyosimamiwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi.

 Sisi Vijana wa CCM, tunaitaka serikali iwatendee haki Vijana hawa wa Watanzania Masikini waliochagua ku sucrify Chaguzi za masomo mbali mbali na kujiunga na Kozi hii iliyobuniwa na Uongozi wa serikali ya Chama chetu. Kwa namna yeyote Ile vijana hawa hawana makosa.
Tatu,Serikali Itoe tamko kabla ya Suala hili halijafanyiwa upotoshaji mkubwa zaidi na kusababisha Matatizo ya kisaikolojia Kwa Vijana na wazazi husika wa kadhia hii.
 
Nne, Serikali kupitia wizara husika itoe muelekeo mahususi juu ya Namna gani imejipanga Kwa mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu juu ya kuhakikisha walimu wa Sayansi wanapatikana katika shule zetu za kata nchi nzima na Hivyo kuunga mkono juhudi zilizofanywa na wanachi za kujenga Maabara katika karibu kila shule ya sekondari nchini.

 Mwisho, Tunaomba serikali kupitia wizara ya Elimu ishirikishe wadau wa pande zote kushughulikia Suala hili na kutoa kauli moja ili kutoa muelekeo wa pamoja tofauti na ilivyo sasa Kwa kila mdau kutoa kauli yake na hivyo kuacha umma kuwa katika mkanganyiko .

 Mohamed Nyundo (MNEC) M/kiti UVCCM(M) Pwani.

Chapisha Maoni

0 Maoni