Jumatano, 15 Juni 2016

UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA SHINA LA UVCCM MAKAO MAKUU Jana tarehe 14/06/2016 umefanyika Uchaguzi wa Shina la Ofisi ya Makao makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.
Uchaguzi huu umehudhuliwa na Kaimu Katibu Mkuu akiwa kama Mgeni Rasmi lakini Pia akiwa kama Mjumbe katika Uchaguzi huo!

Uchaguzi umefanyika na Kulikuwa na Wagombea Watatu ambao ni.
1. John Luputi
2. Mwanaisha Banala Hassan
3. Mwarami Abdallah Kindumbo

Uchaguzi huu ulikuwa na Wajumbe 27 Wamepiga Kura wote na Hakuna Kura iliyoharibika.
Matokeo yakawa hivi.
1. John Luputi (15)
2. Mwanaisha Banala Hassan. (3)
3. Mwarami Abdallah Kindambo ( 11 )

Na Msimamizi wa Uchaguzi huo Ndg Beatrice akamtangaza Ndugu JOHN LUPUTI kuwa Mwenyekiti wa Shina la UVCCM Makao Makuu.
Baada ya Kutangazwa Mwenyekiti Luputu akazungunza na Wajumbe nakuwaahidi kuwapigania katika Kila Mahitaji yao ya kila siku.

 Lakini kawaomba Wajumbe hao ambao niwaajiliwa wa UVCCM kuwa Wachapa kazi ili Kukijenga chama.

Apo awali Kaimu Katibu Mkuu alikaribishwa na Mkuu wa Utawala wa Jumuiya ya Vijana Ndg. Omar Ngwanangwalu Ambae pia alisema Nimuhimu kujituma nakuchapa kazi kwa Juhudi Zote ili Kuijenga Jumuiya ya Vijana.

Kaimu Katibu Mkuu Ndg. Shaka Hamdu Yeye alisisitizia Zaidi Kuwa Zama za Umoja wa Vijana za Leo Si Maneno ila Kazi tu!

Nakumuomba M/kiti Mpya kuzingatia Kazi zaidi kuliko maneno mengi.
Mwenyeti huyo Mpya ameanza Kazi yake Maraa tu baada ya Kuchaguliwa.
Ivo Shina la UVCCM Makao Lina Viongozi Wafuatao.
1. M/Kiti ni John Luputi
2. Katibu ni Theresia Ibada.
Wajumbe ni
1. Muhhamad Nassor
2. Mwarami Kindumbo
3. Issa Nyanza

Uchaguzi huu uliongozwa na M/kiti wa Muda Bi. Mwajuma Rashid.
Wasimamizi wakuu ni Theresia na Beatrice kutoka Shina la Makao makuu ya Ofisi Ndogo ya Chama cha Mapinduzi Lumumba.

Hapa Kazi Tu.

Kidumu chama cha Mapinduzi.
Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi ama mawakala wa Wagombea walipokuwa wakihesabu Kura.

Dada Mwanaisha Banda Hassan akipiga Kura.

Mkuu wa Utawala UVCCM Taifa Ndg. Omar Ngwanangwalu Akipiga Kura.

Kaimu Katibu Mkuu Ndg Shaka Hamdu akipiga kura.

Dada Vaileth Violet Sambik Mjumbe akimuuliza Swali Mgombea Mwalami.

Dada Jane Kinunda Sekretari wa Kaimu Katibu Mkuu Akiomba Mwongozo kwa Mwenyekiti wa Muda kuhusu Mgombea Mwalami ambae Alidai anamashaka na Uraia Wake! (hapa alikuwa anachomekea tu).

Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu akizungu katika uchaguzi huo.


Mkuu wa Utawala Omar Ngwanangwalu Akizungunza katika Ukumbi wa Uchaguzi.

Wagombea walitambukishwa.

Mgombea Mwalami akitambukishwa.

Mgombea Mwanaisha akitambulishwa.

Kutoka Kushoto ni Mwajuma M/kiti wa Muda wa Uchaguzi, Kati ni Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu anaefuata ni Mkuu wa Utawala na alieinama ni Ndg Melele.Mwenyekiti akisalimia Wajumbe.

Karatasi ikionysha Matokeo.

Mkuu wa Idara oganaizesheni akisema neno mbele ya Mwenyekiti aliekaa katikati.

Wagombea wakiwa wamekaa pamoja.

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu