Ijumaa, 24 Juni 2016

UVCCM na BAVICHA hapatoshi sasa

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka. 
 


Na Mwandishi Wetu, Iringa


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM) umelitahadharisha na kusema Baraza la Vijana la Chadema halina uwezo, ubavu wala uthubutu wa kuuzuia au kuukwamisha kwa namna yoyote mkutano mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu .


Aidha umoja huo umesisitiza  kwamba mkutano huo utafanyika vile vile  kama ilivyopangwa hivyo Bavicha kama kweli ni vidume wa mbegu wajitokeze ili wakione cha  matema kuni.


Msimamao huo umetangazwa  jana na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa Iringa katika jengo la CCM akiwa njiani kuelekea Ihemi mkoani hapa. 


Shaka alisema UVCCM wako tayari kuidhihirishia dunia kwa kuwatia adabu Bavicha ikiwa siku moja watajaribu  kufanya jambo lolote  linalotishia kuhatarisha usalama au ustawi wa maendeleo ya kisiasa ya CCM kwa saa, siku,  wakati na mahali popote. 

  
Alisema siku moja ikitokea Bavicha kutenda jambo lolote la hujuma au kudhuru, UVCCM haitaomba kibali au ruhusa ya viongozi wa juu wa  CCM  badala kitakachotokea  dhidi yao  ni matokeo mabaya ambayo  yatakayongia katika vitabu vya historia. 


"Tunalaani tishio la kipuuzi la Bavicha , tunataka kuona jeuri yao, ubavu na misuli yao ili  kuuzuia mkutano  maalum wa CCM Julai 23 mwaka huu, watakavyokuja sivyo watakavyorudi, wajaribu ili wakione kipurepure cha marombe siku  watakapojaribu."alisema Shaka. 

Tamko hilo  la Shaka linafuatia kauli iliotolewa hivi karibuni na viongozi wa Bavicha wakitishia kufanya lolote ili kuhakikisha mkutano mkuu maalum wa CCM hautafanyika mkoani Dodoma mwezi  ujao.

Aidha Kaimu huyo Katibu mkuu alisisitiza  ikiwa Bavicha na Chadema wameshindwa kuendesha siasa za kiungwana zinazoheshimu na kufuata misingi ya kikatiba na kisheria , UVCCM haitashindwa kutia ndimi zake puani au kubadili kurasa za historia mwanana iliopo . 

Shaka aliwataka Bavicha kuacha siasa za mikwara, vitisho, kutishia usalama na amani ya nchi kwa kuijifanya vijogoo wakati hawana lolote wanaloweza aidha kuzuia,  kujenga au kubomoa .

"Bavicha lingekuwa Baraza makini, lenye vijana wa kisasa wenye maarifa , upeo na upembuzi wa kisiasa , wasingekaa bila ya kuwaasa au kuwaonya wabunge wao wanaoshinda kwenye viwanja vya bunge wakipuuzia dhamana ya kuchaguliwa   au kujua maana na mantiki ya misingi ya  uwakilishi bungeni "alieleza  

Alisema kukaa kimya kwa Bavicha bila kuonyesha na kutowaelekeza viongozi wao ni wazi  Baraza hilo limefiisika, halina vijana wenye ujasiri,  maamuzi wala  weledi hivyo ni sawa  na mbwa anayebweka nyakati za usiku  akiwa hana meno ya kuuma .


Hata hivyo Shaka aliwataka makatibu wote wa mikao UVCCM na wilaya kuendelea na maandalizi ya kuwanoa kiitifaki  Green Guard ambao watakuwa  macho kwa kazi malum za kulinda mali za chama na usalama wa viongozi toka sasa hadi kumalizika kwa mkutano maalum Julai 23 mwaka huu .

Hapa ndipo utakapoona tafauti ya CCM na Vyama vingine,  sisi ni chama cha Siasa wenzetu wana mashirika ya kisiasa lazima tuwaoneshe wananchi utofauti wetu  endeleeni kujiandaa vizuri kimkakati ili tufanikishe mkutano mkuu wetu kwa mafanikio makubwa ili tuzidi kuidhihirishia dunia kuwa CCM ni chuo cha demokrasia hakuna mwenye ubavu wa kuzuwia mkutano mkuu maalum Dodoma  na kama yuko anaetaka kujaribu UVCCM tunamwambia ajaribu aone ifike pahala kuwe na kikomo paka hachezewi sharubu kirahisi rahisi" alionya huku akielekeza shaka.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu