Alhamisi, 28 Julai 2016

KOMREDI JAPHARY MGHAMBA; JK TUTAKUKUMBUKA

Ndg. Japhari Mghamba Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Mwanga akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.
Napenda kutumia nafasi hii kwanza kumpongeza mwenyekiti wetu mstaafu Baba wa diplomasia na Siasa Afrika, Comrade Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuhitimisha salama Utumishi wake ndani ya chama na serikali na kuamua kwa ridhaa yake kukabidhi kijiti cha uwenyekiti wa chama chetu kwa Dk. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti wetu wa awamu ya tano.

Bila kigugumizi na bila kwikwi sisi Vijana wa CCM wilaya ya mwanga Mkoa wa Kilimanjaro tunapenda kuwa wa kwanza kumpongeza sana Dk. JK kwa kazi nzuri na nzito ya kukitumikia chama chetu kwa uaminifu mkubwa huku akimtanguliza Mungu mbele,pamoja na changamoto zote tulizopotia kama chama Dk. Kikwete alibaki kuwa Kiongozi imara asiyeyumba ama kutikiswa kwa chochote jambo lilituletea heshima kubwa kitaifa na kimataifa na mafanikio makubwa ya kiuchumi,kisiasa,kijamii,kidiplomasia na kifikra..

Tunapenda kumuhakikishia kuwa heshima na Imani kubwa aliyoijenga Ndani na nje ya chama chetu hatutaiacha iyeyuke tutaihifadhi kama dhahabu maana ni jambo la nadra sana kupata chama kikongwe kinachoimarika kila baada ya Uchaguzi lakini kwa umakini na uimara wa viongozi wake hilo ndio jibu la mafanikio ya CCM barani Afrika na Dunia kwa ujumla.  Tunapenda kumtakia kila la Kheri katika ustaafu wake, sisi Vijana wa Mwanga tunaamini kuwa Dk. Kikwete amestaafisha mwili wake lakini fikra, mawazo na moyo wake wa kukitumikia chama na Taifa letu bado ungalipo.

Nitumie pia fursa hii adimu na adhimu kumpongeza sana Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi mkubwa wa heshima alioupata kwa kupigiwa kura za ndio kwa 100% hii ni heshima kubwa aliyoipata,ni Imani isiyokuwa na chenga aliyoipata na ni ushindi usio na kihoro,Tunaamini heshima,Imani na ushindi huo alioupata Dr.Magufuli ni kutokana na Kazi nzuri aliyoifanya, na anayoifanya ya kulijengea heshima Taifa letu,ya kutekeleza kwa kasi ilani ya Uchaguzi ya CCM na namna anavyoguswa na matatizo ya wanyonge na masikini wa Taifa hili katika masuala mtambuka ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.
Mapenzi na moyo aliokuwa nao kwa Taifa letu na chama chetu. Ushindi huu ni salaam kwa wanafiki,wazandiki,wazushi,waongo na wafitini wasiokitakia mema chama chetu.

Umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Mwanga tumeupokea ushindi wa Dk.Magufuli kwa furaha isiyo na kifani. Tunaamini kuwa ilikuwa wakati sahihi na muafaka kwa sasa chama chetu kuongozwa na Dk.Magufuli.

Kubwa zaidi lililotukosha ni Hotuba nzuri na nzito aliyoitoa Jana wakati wa kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa. Sisi tumeichukua hotuba hiyo kama dira na taswira ya chama chetu kwa Kipindi cha miaka mitano,Tunaamini kwa mapenzi,hari,moyo,uzalendo na uthubutu aliokuwa nao kwa Taifa letu wa kutamka na kutenda tutafika tukiwa na chama imara,makini na chenye uwezo madhubuti wa kuiongoza dunia katika demokrasia ya kweli.

Hotuba ile ya Jana ya Dk. Magufuli ni Tangazo la vita Ndani ya chama dhidi ya vilaza,wababaishaji,wasaliti,wanafiki,wabeba mikoba,wasakatonge,mavuvuzela,matapeli,mafisadi,wanyang'anyi wa Mali za chama,wabadhilifu na wavivu. Tunaamini kuwa sasa ni wakati wa chama kushika hatamu na ni muda a wanyonge na masikini kunufaika na jasho la kukitumikia chama chao.. Ile kasumba ya watu kupiga Dili Dili,udalali wa kisiasa,iyenaiyena na ujujaree uliokithiri na usiokua na tija katika chama sasa ndio muarobaini wake.

Pamoja na pongezi zote hizo nitoe ushauri Wangu pia kwa nwenyekiti wetu mpya kuwa sasa tuanze kujenga Chama kiuchumi,kisiasa,kidiplomasia,kijamii na hasa kubadili mfumo kutoka katika iyenaiyena na kujijenga kitaasisi lazima sasa tuwe na makatibu wa mikoa na Wilaya wenye uwezo,Sifa na wabunifu,uimarishaji na uboreshaji wa mishahara ya watumishi,ushimamizi wa mali za chama,kuimarisha Mahusiano ya kijamii katika vyanja zote za kimichezo,kidini,NGO's, vyombo vya Habari nk,kuwa na watumishi wachache wenye tija,kufufua Vyuo vya chama,kuimarisha jumuiya za chama,kuipa nguvu na kukiboresha kitengo cha Maadili na Usalama kuwa idara kamili iliyohuru na inayojiendesha kimkakati,kuviimarisha Vyombo vyetu vya chama kuendana na wakati ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa TV ya chama,kuanzisha benk ya kifedha kwaajili ya mikopo yenye riba nafuu,kupitishia mishahara ya watumishi,kuongeza heshima ya mabalozi wetu ikiwa ni pamoja na kuwapa posho na motisha,kuingia ubia na vilabu vikubwa duniani vya mpira kujenga viwanja vya kisasa vya mpya,kuimarisha bendi ya chama nk... Yapo mengi ya kushauri lakini kwa uchache ningependa niishie hapo.

Mwisho kabisa nimpongeze Comrade Kinana kwa heshima kubwa aliyoipata ya kuteuliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa natambua haikuwa rahisi ila ni kutokana na uimara,Kazi,moyo na ujasiri mkubwa aliokuwa nao Comrade Kinana wakukijenga chama chetu katika hali zote jua,mvua,chumvi na sukari amekitoa chama chetu katika milima na mabonde..tunaaamini tukiendelea kumpa ushirikiano tutafika.

Mungu awaongoze vyema viongozi wetu katika majukumu yenu,Kheri na Baraka ziwafunike Inshaallah.

Imetolewa na ;
JAPHARI KUBECHA MGHAMBA

MWENYEKITI WA VIJANA WA CCM WILAYA YA MWANGA,KILIMANJARO.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu