Unordered List


UVCCM:BAVICHA msithubu, mtajuta



SHAKA: asema wako fit kuikabili CHADEMA.

RPC: Hakuna wa kuzuwia mikutano wa CCM.

Na Mwandishi Wetu, Dar
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi umesema Bavicha wanaweza kujutia  uamuzi wao ikiwa watathubutu kwa namna yoyote kuvuruga, kudhuru au kutimiza mpango wake wa hujuma dhidi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM  julai 23 Mwaka huu .

Pia Umoja huo umesisitiza  ikiwa vijana wa Chadema watampiga hata mjumbe mmoja au kiongozi wa CCM ,  UVCCM haitasita kupita juu ya nyayo walizopita wapiganaji wa maumau ya  Kenya ili  kukihami chama chao.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka aliyasema hayo jana wakati akitoa msimamo wa UVCCM  siku moja baada ya BAVICHA kutoa tamko la kuandaa vijana 2,000 ili kulisaidia jeshi la polisi  nchini kuzuwia mkutano mkuu wa CCM  uliopangwa kufanyika mjini Dodoma Julai 23 mwaka huu.

Alisema kama  Bavicha wataamua kushiriki  siasa za kishetani  zile za hujuma na kutiashana maisha , kujenga taharuki katika jamii au  kuiingiza nchi katika  vurugu, watawakabili kwa  nguvu za umoja wao.

Aliongeza kuwa  Baraza hilo la Vijana  limeelekezwa na viongozi wake  waanzishe siasa za vurugu , mapigano au ghasia kama njia ya kujenga kisiasa, UVCCM itajibu mapigo yote  kwa gharama ile ile watakayoitumia .

"Hatutaona muhali kupita  njia zilizotumiwa na Mau mau wa Kenya ili kukihami chama chetu, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi  na heshima yetu"alieleza Kaimu Katibu Mkuu .

Shaka akitoa mfano alisema mataifa yote duniani yalioendelalea kiuchumi na kidemokrasia yamfikia malengo yake baada ya kutenganisha vipindi vya siasa na vya kujijenga kiuchumi hivyo Tanzania nayo haitakubali kuendeleza malumbano ya kisiasa na kufuja wakati wa kujipanga kimkakati ili  kuyasaka  maendeleo.

Pia kiongozi huyo wa uvccm alisema jumuia yake haitavijulisha vyombo vya ulinzi  kufuatia tishio la Bavicha badala yake watakachokifanya ni kuendeleza na  maandalizi yao ili kujikinga na kujilinda.

"Bavicha wache siasa za kitoto  serikali ilizuia mikutano na shuhuli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani na kusababisha vurugu si mikutano ya kikatiba"

Alifahamisha kuwa Chadema na viongozi wake wafilisika kisiasa ,sasa wanashawishi vijana wao wajiingize katika matatizo wakifikiri hiyo njia ya kujinasua, kwa vile chama Chao  kimepoteza dira na uwezo wa kushindana na CCM kwa hoja, wakitamani  wajue  watambulia majuto.

 "Mikutano CCM ni wa uteuzi wa Mwenyekiti wa Taifa ambao ni wa kikatiba  tofauti na mikutano mengine kama ule wa ACT Wazalendo  uliokuwa na lengo la kufanya uchochezi  dhidi ya bajeti na mikutano iliyotangazwa na CHADEMA  ikiwemo iliyohusisha kukutana na wanafunzi  ilikuwa na malengo ya kufanya uchochezi  huku wakijificha kwenye kivuli cha mahafali
wasipotoshe watu
Rais Yupo Sahihi haiwezekani nchi mwaka mzima iwe katika siasa tu " alisema Shaka

Shaka ameendelea kuwahimiza makatibu wote wa mikoa kuendeleza kuwaandaa vijana wa ccm kinidhamu,  kimkakati na kisaikolojia kuelekea mkutano mkuu julai 23 Mwaka huu utakaofanyika mkoani Dodoma .

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma  Lazaro Mambosasa  alisema vijana hao hawana uwezo kuzuwia mkutano huo .
Kamanda Mambosasa alihoji kuwa baraza hilo linataka kuzuwia mkutano huo wakiwa kama nani?  huku akiweka wazi kuwa jeshi la polisi limejipanga kikamilifu na halina shida katika suala la ulinzi wa mkutano huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni