Mkuu wa Wilaya Rombo Mhe. Agness Elias Hokororo akiambatana na Das wake Mhe. Abubakar D. Asenga akiongoza kikao na wafanyakazi wa TRA na Uhamiaji katika mpaka wa Tanzania na Kenya Wilaya ya Rombo. |
Mkuu wa Wilaya Rombo Mhe. Agness Elias Hokororo akiambatana na Das wake Mhe. Abubakar D. Asenga akiongoza kikao na wafanyakazi wa TRA na Uhamiaji katika mpaka wa Tanzania na Kenya Wilaya ya Rombo. |
DC Hokororo atembelea Mpaka wa Tanzania na Kenya,ofisi za TRA na uhamiaji Kata ya Holili-Rombo
Leo Jumanne august 2016.
Mkuu wa Wilaya alifika katika ofisi hizo kwa lengo la kujitambulisha na kufikisha ujumbe kwa watendaji wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
"...nyie wote mnajua kuwa usafirishi mahindi umezuiwa kwa sasa,watu wameacha kupitishia sehemu zingine wanakuja hapa Holili kwa kuwa mnawatengenezea mazingira,naambiwa kuna magari ya wakubwa ,wakubwa ndio nani? Kamateni tu ata kama gari ya DC Rais alishasema maana nimeshaona ona hapa vimualiko vya hawa watu wanaotajwa kuwa ni wakwepa kodi......SIDANGANYIKI..... kuna njia za panya 264 zinapitisha Magendo hapa.....uhamiaji timizeni wajibu wenu na naomba taarifa za wote wanaowakwamisha...."
Mh Dc alionya pia juu ya taarifa za kijiji cha Holili vijijini ambapo karibu asilimia 80 ya wakazi Si watanzania(wakamba) wakuzaliwa wanaopiga kura Kenya na Tanzania.....pia alitaka kujua hatua ambazo uhamiaji wanapaswa kuchukua hasa baada ya Tanga Cement kulipa fidia wakazi hao ili wahame sememu ya uwekezaji...hali iliosababisha wakazi hao kuingia ndani zaidi ya Rombo na kuchanganyika na Watanzania bila kufata utaratibu wa kihamiaji ndani ya Afrika ya mashariki
Mh Hokororo aliulizia pia suala la matumizi ya EFD(mashine za Kutoa risiti kwa umeme) kwa tozo za uhamiaji kwanini hadi sasa hazijaanza kutumika ? Na alijibiwa kuwa lipo kwenye utaratibu na atapitia tena kufatilia ili kukuza zaidi mapato ya serikali
Kituo cha Holili kwa mwezi wanakusanya karibu Billion 5 hivyo ufanisi ukiongezeka serikali yaweza kupata mapato zaidi ya hayo
Mh Dc alitaka taarifa toka kila kijiji cha mpakani kwa wakati na maiti zote zinazopita hapo mpakani zionyeshe utaifa wa marehemu na uchunguzi wa kina ufanyike na wataalamu ili kupunguza hatari ya maambukizi
Suala la wanywaji pombe muda wa kazi hasa maeneo ya mpakani pia lilitahadharishwa na Mh Dc na kuwa yeye ni mgeni ila atakula sahani moja na wazembe wanaoshiriki katika magendo yote.
ROMBO YENYE NEEMA ZAIDI INAWEZEKANA
HAPA KAZI TU
0 Maoni