• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ijumaa, 30 Septemba 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA RASMI AHAMIA MKOANI DODOMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa Dodoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 2016.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa Manispaa ya Dodoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 
 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama Kikundi cha Ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba 30, 
 2016.

Waziri Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.


Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri MkuuWaziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba  huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote."


“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipoAmewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.


"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa  viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.


"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma," amesema.Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA

IJUMAA, SEPTEMBA 30, 2016.
Share:

WAZIRI MKUU APOKEA MICHANGO ZAIDI YA SH. MILIONI 760

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mbunge wa Afrika ya Mashariki ShyroseBhanj ukiwa ni mchango wa waathiri wa tetemeko, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016.Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji , CharlesMwijage.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita .

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea zaidi ya sh. milioni 760 zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu. 
Amepokea misaada hiyo kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali likiwemo kundi la wanawake New Millennium  linaloundwa na wake wa viongozi wa Serikali walio madarakani na waliostaafu.
Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo jioni (Alhamis, Septemba 29, 2016) kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam pamoja na makazi ya Waziri.

Miongoni mwa waliokabidhi misaada hiyo ni pamoja Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita sh. milioni 10, Kampuni ya mabati ya ALFA imekabidhi mabati yenye thamani ya sh. milioni 50 na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sh.milioni 100.
Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu kampuni ya vinywani baridi ya Pepsi Cola, Bw. Avinash Jha amekabidhi sh.milioni 50, kampuni ya Round Table pamoja na wadau wao sh. milioni 57,kampuni ya Wool Worth  sh.milioni 20 na Jumuiya ya Waislam (FIRDAUS) imetoa viti 15 vya walemavu.
Aidha, kampuni ya Trans Ocean Supplies LTD imetoa sh. milioni 20, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza amekabidhi sh. milioni 18.681,Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji amekabishi sh. milioni tano.

Pia Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta Tanzania kimekabidhi sh. milioni 415.8, kundi la mtanzao wa kijamii la Whatsapp la Papaso, D’jaro Arungu limekabidhi sh.520,000 na kampuni ya mafuta ya Camel iliyokabidhi mifuko 1,000 ya saruji.

Jumuia ya Wanataaluma ya Vyuo Vikuu vya Umma Tanzania (ASAs) imekabidhi sh. milioni 7.5, Umoja wa Wamiliki wa Maduka ya Dawa Muhimu Tanzania umekabidhi dawa zenye thamani ya sh. milioni tano pamoja na Eric Shigongo wa Global Publisher amekabidhi mabati 500 yenye thamani ya sh. milioni 10.

Waziri Mkuu amewashukuru wadau wote kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Tunashukuru sana kwa michango yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa. Amesema.

Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa),au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
Share:

MWENYEKITI NJARU ATEMBELEA VIJANA WA HALAIKI YA UZIMAJI WA MWENGE MKOANI SIMIYU

 Vijana wa Halaiki ya Siku ya Kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu wakiendelea na Mazoezi.
   Katibu Hamasa sera utafiti na mawasilianoMkoa Simiyu ndg Mayunga Kidoyayi pamoja na katibu Uvccm wilaya ya Bariadi ndg Joel Makwaia wakimpa maelezo ya kina kwa Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Simiyu(MNEC) na Mbunge wa jimbo la Itilima Ndg. NJALU SILANGAalipo tembelea eneo wanalo fanyia Mazoezi Vijana wa Halaiki.
Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa Simiyu  na Mbunge wa Itilima ndg NJALU SILANGA (Mnec)akizungumza na watoto watakaocheza halaiki kwa ajili ya zoezi la uzimaji wa Mwenge wa uhuru Mkoani  Simiyu.
Share:

Alhamisi, 29 Septemba 2016

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri Mkuu Mhe:Kassim Majaliwa Kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba,29,2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba,29,2016.

 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumzia Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu kuridhia Ujenzi wa Bomba la Mafuta leo Septemba,29,2016.

picha na Michuzi Blog

Share:

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA HATI YA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA UINGEREZA HAPA NCHINI SARAH CATHERINE COOKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke kufatia mchango wa Waziri Mkuu wa Uingereza alioutoa kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kiasi cha Paundi za Uingereza Milioni 2.3 sawa na Takribani Shilingi Bilioni sita za Kitanzania


PICHA NA IKULU
Share:

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOA WA GEITA.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb), (Wa kwanza kulia) akipokea maandamano katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  yaliyofanyika mkoa wa Geita. Wa pili kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb) akisalimiana na mmoja wa walemavu aliyejitokeza kushiriki katika maadhimisho ya  Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa, Mkoa wa Geita.
 Mmoja wa watumishi kutoka wizara ya ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano akitoa elimu kwa wanafuzi wa shule ya msingi kalangalala walipotembelea banda la wizara hiyo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa mkoani Geita.
 Kikosi cha Brass Band kutoka Serengeti Mkoani mara kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa yamefanyika mkoa wa Geita.

Waendesha pikipiki (boda boda) mkoa wa Geita wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kitaifa.

Share:

RAIS DKT MAGUFULI ALIVYOZINDUA RASMI NDEGE MBILI MPYA ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KWA AJILI YA ATCL JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam  Jumatano Septemba 28, 2016.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam  Jumatano Septemba 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam  Jumatano Septemba 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kwenye ndege mojawapo na kuelekea ingine baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine waandamizi katika picha ya kumbukumbu na watumishi na viongozi wa ATCL mara baada ya Rais Magufuli kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam  Jumatano Septemba 28, 2016. 

PICHA NA IKULU
Share:

BALOZI GERTRUDE MONGELLA: TANZANIA HAKUNA UKANDAMIZAJI WA HAKI ZA BINADAMU

BALOZI GERTRUDE MONGELLA KATIKATI  KUSHOTO NI  KATIBU WA UVCCM WILAYA YA KINONDONI  RASHIDI SEMINDU   KULIA NI MCHUMI WA UMOJA WA WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM GASTON ONYANGO

  Na Nassir Bakari

 Waziri mstaafu na Mwanadiplomasia maarufu duniani, Balozi, Gertrude Mongella, amelaani kitendo cha baadhi ya wanasiasa kupotosha ukweli na kusema Tanzania kuna ukandamizaji wa haki za Binadamu.

Balozi Mongella aliyasema hayo nyumbani kwake, Makongo Juu jijini, Dar es Salaam alipotembelewa na viongozi pamoja na wanachama wa Umoja wa vijana(UVCCM), wilaya ya kinondoni.


Balozi Mongella alisema nchi yetu ni nchi yenye Amani na anasikitika kusikia wanasiasa wakisahau kwa makusudi juhudi za kupigania Uhuru zilizofanywa na wazee wetu.


“Kuna msemo wa Kiswahili usemao hakutukanae hakuchagulii tusi na hawa wanasiasa wasiojua nini maana ya siasa watasababisha tuendelea kutukanwa na mataifa ya nje, na hatimaye kupelekea kutoweka kwa urithi wetu wa umoja na mshikamano," alisema Balozi Mongella na kuendelea:-


“Swala la haki za binadamu nimelitafakari kwa muda mrefu sana na nilipokuwa Beijing nimejifunza kwamba Tanzania ni nchi inayothamini haki za binadamu kwa kiasi kikubwa kuliko nchi nyingi duniani, mfano mzuri ni uwiano wa wanawake na wanaume kwenye uongozi nchi yetu ina uwiano mzuri sana na je hiyo sio haki ya binadamu,?  tatizo wanasiasa wa Tanzania wanacopy na kupaste kutoka kwenye democracy tuliyoletewa na hawakujifunza kushindwa," alisema Balozi Mongella.


Pia Balozi Mongella aliwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha kuilaumu serikali kwa kukosa ajira na kuwataka wajifunze kinachofanywa na  Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa ujumla na kuendana na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.


Share:

Jumanne, 27 Septemba 2016

UVCCM TAIFA KUTUMA MKAGUZI WA HESABU ZA MALI ZA JUMUIYA HIYO ZILIZOPO ARUSHA


Na Woinde Shizza,Arusha
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM, taifa itatuma mkaguzi wa hesabu na mali  za jumuia hiyo mkoa wa Arusha, katika kipindi cha wiki mbili kuanzia Septemba 27 mwaka huu ili kupata ukweli zilipo shilingi milioni 112.8 za umoja huo zinazokusanywa kila mwaka kutokana na kodi ya maduka.


Makamu mwenyekiti UVCCM, Taifa, Mboni Mhita, aliyasema hayo jana mara baada ya kikao na wajumbe wa baraza la UVCCM ,mkoa wa Arusha, kilichofanyika ukumbi wa ccm ,mkoa na baada ya muda huo kamati ya taifa ya UVCCM, itarejea mkoani Arusha kufanyia kazi yaliyobainishwa na mkaguzi wa hesabu.


Mhita,ambae anaongoza kamati ndogo ya watu watatu ya UVCCM,taifa,alisema anawashangaa wajumbe wa baraza hilo kushindwa kuchukua hatua na kusimamia jumuia hiyo hadi washikane mashati wakati wao wakiwepo na sasa wanagombea vibanda vya maduka ambavyo hawakuvijenga na wala hawajajenga vipya.


Mhita,  alisema baadhi ya wajumbe wa baraza la UVCCM, Mkoa wa Arusha, hawaelewi  maana ya UVCCM, majukumu yao kwa kuwa hawajasoma kanuni za umoja huo  na wameingia kwenye uongozi bila kuwa na sifa na ndio chanzo cha migogoro.


Wajumbe hao walikutana  na UVCCM kwenye mchakato  wa kugombea uongozi  na hawajosoma kanuni na katiba ya UVCCM hivyo kuwepo mitafaruku ndani ya umoja huo mkoani Arusha, ambayo inakwamisha maendeleo na ufanisi  wa shughuli za umoja huo.


 Alibanisha kuwa  baraza lazima libebe lawama  kwa kushindwa kusimamia majukumu kutokana na kushindwa kuendana na sera  za ccm kutokana na kukosa uadilifui, na kutokutambua majukumu yao.


Kamati hiyo ndogo inafuatilia mgogoro wa UVCCM ,mkoa wa Arusha, ambapo  miongoni mwa majukumu ya kamati hiyo ni kuwasikiliza wajumbe wa baraza hilo kutokana na mgogoro uliojitokeza  hivi karibuni.


Mhita, alilitaja jukumu lingine la kamati hiyo ndogo kuwa ni kupatiwa nyaraka za mikataba ya wapangaji wa maduka yote ya UVCCM, mkoa huo.

Aidha alisema kuwa   baadhi ya viongozi wa baraza hilo waliandika barua ya kuwatukana na kuwadharirisha viongozi wa UVCCM taifa lakini leo walipoulizwa kwenye kikao hicho wamekana saini zao.


Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa UVCCM taifa, Shaka Hamdu Shaka, alisema   UVCCM ni taasisi kubwa ya Chama cha Mapinduzi hivyo lazima wazingatie  heshima, umoja  na ushirikiano  kwa kuwa ndizo nguzo za uvccm.

Amewaambia kuwa UVCCM, Inaongozwa na  kanuni, mbili za Utumishi na  Utawala  ,taratibu za fedha , maadili ya viongozi


Alisema kilichotokea kwenye uongozi wa UVCCM, mkoa wa Arusha ni kutokufuatwa kwa kanuni ,taratibu  na miongozo ya jumuia hiyo.


Alibainisha kuwa  ukiukwaji huo wa kanuni kumesababisha mgogoro wa uongozi uliopelekea aliyekuwa mwenyekiti wake, Lengai kusimamishwa uongozi huku aliyekuwa katibu wa mkoa Ezakiel Mollel, nae akiondolewa kutokana na kukaidi maelekezo ya mwajiri wake kuhamia makao makuu.


Alisema kuwa  anashangazwa kuona UVCCM ikiwa na wajumbe 16 wa kamati ya miradi jambo ambalo ni kinyume na kanuni za UVCCM kwa kuwa hakuna kifungu kinachoelekeza kamati iwe na wajumbe wengi kiasi hicho hata taifa haipo.


Aidha alisema  UVCCM mkoa wa Arusha, inakusanya shilingi milioni 112.8 kwa mwaka makusanyo yanayotokana na maduka yaliyopo kwenye jengo la UVCCM mkoa lakini hazijulikani ziliko.


Awali mjumbe wa kamati hiyo kutoka mkoa wa Lindi,Amir Mohamed,aliwataka wanachama wa UVCCM mkoa wa Arusha, kujenga umoja na,upendo  na kuacha kushughulikiana wao kwa wao na kusababisha migawanyiko ili kuiwezesha jumuia hiyo iweze kufikia malengo na kutimiza majukumu yake ya kisiasa.


Mohamed, alikuwa akitoa salamu za UVCCM taifa, kwenye kikao maalumu cha baraza la umoja wa Vijana mkoa wa arusha, iliyofanyika ukumbi wa CCM, Mkoa kilichokuwa kikisikiliza mgogoro wa uongozi wa jumuia hiyo.


Alisema UVCCM ni tanuru la  kuoka viongozi  na wajumbe wote wa baraza hilo wana wajibu  kufahamu mipaka  na misingi ya uongozi.Alisema  UVCCM,haitawavumilia watakaokiuka  misingi na maadili  itawatimua  hivyo lazima watumie rasimilami za umoja huo walinde zingine

  kwa manufaa  kwa kuwa  UVCCM ni walinzi wa mali za chama na  viongozi wake.
Share:

RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA MRADI UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA FUMBA


 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kulia ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis,akifuatiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohamed
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipanda ngazi ya moja ya nyumba zinazojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo   Bw.Said Salim Bakhresa  wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo
 Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa mashine za kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group N.P.Singh (wa pili kulia) wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum,(katikati) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa na (kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa(kulia) wakati alipotembelea Mtambo wa  kutengenezea lami katika Kampuni ya Ujenzi ya  Azam Group leo wakati  alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi (wa pili kulia) Mtaam wa Mtambo N.P.Singh. (Picha na Ikulu)
Share:

Jumapili, 11 Septemba 2016

UVCCM WATOA POLE KWA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI

TANZIA  YA UVCCM KWA UMMA KUFUATIA TETEMEKO LA ARDHI  HUKO BUKOBA MKOANI KAGERA TAREHE 10 SEPTEMBA 2O16.

Kufuatia  kutokea janga la tetemeko la Ardhi huko Bukoba  Mkoa Kagera ambalo limepoteza maisha ya watu kadhaa, kuharibu mali na makaazi ya wananchi , Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM )tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa .

Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) tumepokea kwa  mshituko  mkubwa tukio hilo kubwa na zito  ambalo  limesababisha kutokea kwa maafa na  hasara ya mali na makaazi ya watu.

Tukio hilo lililotokea  siku mbili zilizopita limeacha misiba, majeruhi na watu kupoteza mali , vitu vyao vya thamani na kuharibu  maakazi ya binadamu ambao  sasa hawana uhakika wa makaazi mengine.

Janga hilo licha ya kuleta majonzi  vile vile limeathiri maisha ya watu  kinadharia na kisaikolojia ikiwemo watu kupata hofu ya maisha yao, limepoteza nguvu kazi ya Taifa yaani vifo na majeruhi wakiwemo vijana, wanawake na watoto .

Katika kipindi hiki kigumu Jumuiya yetu inaungana  bega kwa bega na watanzania wengine kwa kuzipa mkono wa pole familia zote zilizopoteza ndugu zao na pia tukiwafariji wale wote waliopata hasara ya kuharibikiwa nyumba zao na kupoteza mali.

Janga hili ni letu wote, limemgusa kila mtanzania mwerevu mwenye upendo na uzalendo , lazima litukusanye na kutukutanisha tukiwa wamoja ili kuyakabili magumu yote yaliotokea kwa wakati huu.

Tukio hili la kimaumbile ya dunia huwa na athari kubwa, linapotokea  huleta kiza cha misiba na kurudisha nyuma juhudi za watu waliojijenga kimaisha kwa kupoteza mali na rasilimali zao

Tunampa mkono wa pole Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John  Pombe Magufuli kwa tukio hili zito linaloambatana na vifo vya watanzania wenzetu.

Tunawaomba watanzania wenzetu, ndugu na jamaa ambao wamepoteza ndugu zao, watoto na jamaa zao wawe wenye moyo wa subira katika  wakati huu mgumu na wenye huzuni kubwa .

Tunamuomba mungu awepe ustahamilivu, mioyo yao mungu aitie subira na stahamala huku nasi kwa umoja wetu tutakuwa pamoja wakati wote ili kusaidiana na wenzetu ambao wamepata matatizo hayo.

Tunawashukuru na kuwakupongeza viongozi wenzetu  walioko katika maeneo husika  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Kagera Ndg Yahya Kateme  makundi mbali mbali ya vijana yaliyojitokeza kutoa mashirikiano makubwa wanayoendelea  katika janga hili kwa hakika wametuwakilisha vyema vijana wote wa Tanzania nasi kwa mapenzi ya Mwenyezimungu tutafika kuungana nao katika kuwafariji na   kutoa misaada ya kibinadamu.

Huu si wakati wa siasa bali ni kipindi kigumu cha kukabili yale yote yaliotokea na kudhuru au kuharibu taaswira iliokuwepo awali ya ustawi wa maisha ya wenzetu ambao wamepatwa na janga hilo.

Kila kijana mzalendo ni vyema akaenda kuripoti kwa viongozi wa maeneo husika aidha wakuu wa wilaya au mkoa ili kupewa maelekezo na miongozo katika kila hatua ya kusaidiana kwa hali na mali wakati wote hadi hali itakaporejea kama kawaida.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika na watu wake wote.

Ahsanteni

SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)

Kaimu Katibu Mkuu.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu