Unordered List


BALOZI GERTRUDE MONGELLA: TANZANIA HAKUNA UKANDAMIZAJI WA HAKI ZA BINADAMU

BALOZI GERTRUDE MONGELLA KATIKATI  KUSHOTO NI  KATIBU WA UVCCM WILAYA YA KINONDONI  RASHIDI SEMINDU   KULIA NI MCHUMI WA UMOJA WA WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM GASTON ONYANGO

  Na Nassir Bakari

 Waziri mstaafu na Mwanadiplomasia maarufu duniani, Balozi, Gertrude Mongella, amelaani kitendo cha baadhi ya wanasiasa kupotosha ukweli na kusema Tanzania kuna ukandamizaji wa haki za Binadamu.

Balozi Mongella aliyasema hayo nyumbani kwake, Makongo Juu jijini, Dar es Salaam alipotembelewa na viongozi pamoja na wanachama wa Umoja wa vijana(UVCCM), wilaya ya kinondoni.


Balozi Mongella alisema nchi yetu ni nchi yenye Amani na anasikitika kusikia wanasiasa wakisahau kwa makusudi juhudi za kupigania Uhuru zilizofanywa na wazee wetu.


“Kuna msemo wa Kiswahili usemao hakutukanae hakuchagulii tusi na hawa wanasiasa wasiojua nini maana ya siasa watasababisha tuendelea kutukanwa na mataifa ya nje, na hatimaye kupelekea kutoweka kwa urithi wetu wa umoja na mshikamano," alisema Balozi Mongella na kuendelea:-


“Swala la haki za binadamu nimelitafakari kwa muda mrefu sana na nilipokuwa Beijing nimejifunza kwamba Tanzania ni nchi inayothamini haki za binadamu kwa kiasi kikubwa kuliko nchi nyingi duniani, mfano mzuri ni uwiano wa wanawake na wanaume kwenye uongozi nchi yetu ina uwiano mzuri sana na je hiyo sio haki ya binadamu,?  tatizo wanasiasa wa Tanzania wanacopy na kupaste kutoka kwenye democracy tuliyoletewa na hawakujifunza kushindwa," alisema Balozi Mongella.


Pia Balozi Mongella aliwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha kuilaumu serikali kwa kukosa ajira na kuwataka wajifunze kinachofanywa na  Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa ujumla na kuendana na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.


Chapisha Maoni

0 Maoni