Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tano
kutoka kwa Mbunge wa Afrika ya Mashariki ShyroseBhanj ukiwa ni mchango
wa waathiri wa tetemeko, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 29,
2016.Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,
CharlesMwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita .
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amepokea zaidi ya sh. milioni 760 zikiwa ni misaada kwa wananchi
walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba
10, mwaka huu.
Amepokea misaada hiyo kutoka kwa
taasisi na wadau mbalimbali likiwemo kundi la wanawake New
Millennium linaloundwa na wake wa viongozi wa Serikali walio madarakani
na waliostaafu.
Makabidhiano ya michango hiyo,
yamefanyika leo jioni (Alhamis, Septemba 29, 2016) kwa nyakati tofauti
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam
pamoja na makazi ya Waziri.
Miongoni mwa waliokabidhi misaada
hiyo ni pamoja Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita sh.
milioni 10, Kampuni ya mabati ya ALFA imekabidhi mabati yenye thamani ya
sh. milioni 50 na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sh.milioni 100.
Wengine ni Ofisa Mtendaji
Mkuu kampuni ya vinywani baridi ya Pepsi Cola, Bw. Avinash Jha
amekabidhi sh.milioni 50, kampuni ya Round Table pamoja na wadau wao sh.
milioni 57,kampuni ya Wool Worth sh.milioni 20 na Jumuiya ya Waislam
(FIRDAUS) imetoa viti 15 vya walemavu.
Aidha, kampuni ya Trans Ocean Supplies LTD imetoa sh. milioni
20, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza amekabidhi sh. milioni
18.681,Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji
amekabishi sh. milioni tano.
Pia Chama cha Waagizaji
Wakubwa wa Mafuta Tanzania kimekabidhi sh. milioni 415.8, kundi la
mtanzao wa kijamii la Whatsapp la Papaso, D’jaro Arungu limekabidhi
sh.520,000 na kampuni ya mafuta ya Camel iliyokabidhi mifuko 1,000 ya
saruji.
Waziri Mkuu amewashukuru wadau
wote kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango
hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Tunashukuru sana kwa michango
yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo.
Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na
maafa. Amesema.
Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa),au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).
Tetemeko hilo lililotokea
Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na
wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya
Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38
wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji
mkubwa na wanaendelea vizuri.
Pia tetemeko hilo limesababisha
nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi
baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi
126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
0 Maoni