Jumatano, 19 Oktoba 2016

SHARTI JIPYA LAONGEZWA KWA WANAFUNZI KUPATA CHETI DARASA LA SABA

3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba ameanza ziara katika mikoa 10 ya Tanzania yenye changamoyo kubwa zaidi kimazingira ambapo atazungumza na viongozi, kamati za mazingira na wananchi, pamoja na kuendesha zoezi la upandaji miti katika mikoa hiyo.
Ziara hiyo imeanzia mkoani Morogoro Oktoba 16, ambako Waziri Makamba alijionea hali ya uharibifu wa mazingira maeneo tofauti ya mkoa huo ikiwemo vyanzo vya maji na kutoa maagizo kwa mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya wahusika ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika vyanzo vya maji na kuwafikisha mahakamani.
Kwa upande mwingine akiwa mkoani Iringa  Oktoba 19, Waziri Makamba ameeleza kuwa kuanzia mwakani kila Mwanafunzi wa darasa la kwanza akiripoti shuleni atatakiwa kuja na mche wa mti ambao ataupanda na kuutunza kwa miaka yote saba ambayo atakuwa shuleni hapo. Mwanafunzi hatapewa cheti cha kumaliza darasa la saba kabla hajaonyesha mti wake alioupanda alipowasilshuleni hapo. Haya ameyasema alipokuwa akishirikiana na wananfunzi kupanda miti katika Shule ya Msingi Mlandege Mjini Iringa. Ili kutekeleza azma hii ya serikali, Waziri Makamba aliweka wazi kuwa wizara yake itashirikiana kwa karibu kabisa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayemaliza masomo yake bila kuonyesha mti/miti yake.
Katika shule zenye maeneo madogo, Waziri Makamba alisema kuwa miti hiyo itapandwa katika maeneo yatakayoelekezwa na Serikali za Vijiji na Mitaa. Wanafunzi wa Shule za Sekondari nao vivyo hivyo watatiwa kupanda miti  mitatu ambayo watatakiwa kuitunza kwa miaka yote minne wanapoendelea na masomo.
Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa tarehe 5 & 6 Novemba watakutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wenyeviti na Mameya Wote Arusha Kwa ajili ya kuwapa mafunzo na maelekezo mahsusi yanayohusiana na Hifadhi ya Mazingira, ikiwemo upandaji miti na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Chini ni picha 15 kutoka katika ziara hiyo ya siku 16 ambayo leo imeingia siku yake ya tano.
whatsapp-image-2016-10-19-at-9-23-11-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-23-55-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-00-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-05-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-08-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-11-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-13-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-20-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-24-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-31-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-35-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-39-am-1 whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-39-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-40-am whatsapp-image-2016-10-19-at-9-24-41-am
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu