Unordered List


FINAL ZA NJALU CUP JIMBO LA ITILIMA MKOANI SIMIYU SIKU YA VIJANA KITAIFA

Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde alikuwa mgeni rasmi katika Mwisho(final) mashindano ya mpira wa miguu NJALU CUP zilizofanyika jana katika jimbo la Itilima wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu. 

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa udhamini wa Mbunge wa Jimbo hilo la Itilima Mhe Njalu Daudi Silanga. kwa mwaka huu yamekwenda sambamba na siku ya Vijana kitaifa.

Katika final hizo pia zilihudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka pamoja na viongozi mbali mbali.

Mgeni rasmi wa NJALU CUP Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde akiongea na wanaItilima waliojitokeza kwenye mashindano hayo.


Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde akisalimiana na kutambulishwa timu zilizoingia katina final ya Njalu Cup jimbo la Itilima Simiyu.

Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde,Mbunge wa jimbo la Itimila Mhe Njalu Daudi Silanga,Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa na Viongozi wengine wakitoa zawadi ya kombe kwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya NJALU CUP

Chapisha Maoni

0 Maoni