Balozi
wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni amemhakikishia Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa nchi
yake itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri na ya
kihistoria kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali kama hatua ya
kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.
Balozi
huyo wa Italia hapa nchini ametoa kauli hiyo leo 24-Okt-2016
alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
ikulu jijini Dar es Salaam.Balozi huyo Roberto Mengoni ameeleza kuwa
nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo na Tanzania katika sekta
mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia
miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini.
Makamu
wa Rais amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta
mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati
ya Italia na Tanzania.
Amesisitiza
kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kupokea mawazo mazuri ya
kimaendeleo kutoka kwa Serikali ya Italia yatakayosaidia kujenga na
kuimarisha ustawi mzuri katika jamii hapa nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto)
,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto
Mengoni (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es
Salaam .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiagana na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto)
aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam
0 Maoni