Jumamosi, 8 Oktoba 2016

MBUNGE ULEGA AZINDUA KISIMA CHA KISASA KATIKA KIJIJI CHA LUPONDO ,MKURANGA

Mbunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkuranga,Mhe. Abdallah Ulega, amezindua kisima katika Shule ya Msingi Lupondo, kilichojengwa na African Reflection Foundation. 


Akizungumza Mara baada ya kuzindua Kisima hicho, amesema kuwa kijiji cha Lupondo kilikuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu. Amesema kuwa wananchi hao walikuwa wakitafuta maji umbali wa kilomita tano na kufanya kuumiza kichwa katika kuwapata wafadhili wa mradi huo. 

Mhe.Abdallah Ulega amesema katika kipindi cha miezi tisa ameweza kupata miradi ya maji katika vijiji sita na kuahidi kuendelea kutafuta miradi ya maji katika vijiji vilivyosalia.Hata hivyo katika uzinduzi huo Mh.Ulega ametoa msaada wa mifuko 10 ya saruji katika msikiti wa kijiji hicho. 

Nae mratibu wa African Reflection foundation, Shiraz Mohamed, amesema wataendelea kufadhili miradi ya maji katika vijiji vyenye changamoto hiyo. 

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega,(katikati) akikata utepe wa uzinduzi wa kisima jana katika kijiji cha Lupondo.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lupondo kabla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu