Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mongela amewataka vijana kubuni njia
mbalimbali halali za kuwaingizia kipato ikiwemo ujasiriamali badala ya
kukaa bila kazi huku wakijivunia kuwa kwenye vyama vya siasa.
Amesema ni vyema wanaoingia kwenye
siasa wakahakikisha wana shuguli za kufanya ambapo amewasihi
wajasiriamali wakiwemo Machinga kuwa tayari kufanya biashara zao katika
maeneo yaliyoainishwa na kwamba watakaotii hilo, watanufaika moja kwa
moja na mikopo inayotolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Naye Katibu wa UVCCM wilayani
Nyamagana, Odila Batimayo, kwa niaba ya umoja huo, amempongeza Rais John
Magufuli kutokana na utendaji mwema wa kazi ikiwemo kuanza kutimiza
ahadi zake ndani ya miezi tisa ya uongozi wake kama vile ununuzi wa
ndege, mabehewa, ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na mpango wa
elimu bure nchini.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya
Nyamagana, Hussein Kimu, amebainisha kwamba lengo la mkutano huo ni
kuyapongeza makundi mbalimbali yakiwemo machinga, mamantilie na bodaboda
kutokana na mchango wao katika kufanikisha ushindi katika uchaguzi wa
mwaka jana, ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa mkutano huo
wamepata fursa ya kuchangia damu.
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Mhe.John Mongela (katikati), akisaini kitabu cha wageni baada ya
kuwasili kwenye Mkutano wa Baraza Kuu Maalumu la Umoja wa Vijana wa
Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, uliofanyika "Gandhi Hall" Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela, akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, akisoma taarifa ya UVCCM Nyamagana kwenye mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali na Wageni Waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Taswira ya mkutano
wa Baraza Kuu Maalumu ya UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, ikiwa
ni sehemu ya kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya
kuanzishwa kwa umoja huo, "UVCCM DAY" kitaifa.
PICHA NA BMG
0 Maoni