Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla amewaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa Serikali
inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa nchini
hivyo uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na watu wake
hasa katika Nyanja za kiuchumi,
Afya, Mazingira na
mambo mengine ya kimaendeleo.
Aidha, amebainisha
kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu ambapo ameahidi
amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana nao katika kulipitia
ufumbuzi.
Dk.Kigwangalla amewahakikishia
Wanasayansi hao kuwa, masuala yote ya kuimalisha huduma za Maabara katika
ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa akilifanya kila mahala anapokwenda
kwenye ziara zake juu ya
upatikanaji wa
huduma Maabara bora kwenye sehemu za Afya.
“Nimependa maombi
yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za msingi. Suala
hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo vya Afya na Hospitali
zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa sababu nina aamini kutoa
huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti za Maabara ni kuchezea afya za
watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na huduma bora za Maabra zetu na suala hili
tutakaa mimi na Mh. Waziri kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema
Dk.Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wanasayansi watafiti (Hawapo pichani) walioshiriki kongamano la 30 Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kongamano hilo la siku tatu
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk.
Mwele Malecela akielezea machache kabla ya kumwalika mgeni rasmi kufunga
mkutano huo
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla akimpa shada la maua mmoja wa Staff member kwa namna walivyoweza
kuandaa kongamano hilo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi shada
la maua mmoja wa wafanyakazi wa NIMR kwa namna walivyoweza kufanikisha shughuli
hiyo.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla
akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo
zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo.
0 Maoni