Unordered List


RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MFALME WA MOROCCO MOHAMED VI KATKA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM


Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI leo tarehe 27 Oktoba, 2016 ameondoka Jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar.

Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI ameagwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliyewasili nchini tarehe 23, Oktoba 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na pia viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mtukufu Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi hapa nchini.
  
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Oktoba, 2016.
ano1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akajadiliana jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano4
ano5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano6 ano7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam.
ano8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakiangalia bendi ya matarumbeta iliyokuwa ikitumbuiza katika ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohamed VI aliyemaliza ziara yake ya kikazi na kuondoka jijini Dar es Salaam.
ano10
ano11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakati nyimbo za Taifa zikiwa zinapigwa katika ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Chapisha Maoni

0 Maoni