Rais
 Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa 
Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (kulia kwake) na ujumbe 
wake alipokutana nae Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016. 
Makamu wa Rais wa Cuba, yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu 
yenye lengo la kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na 
Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, utamaduni, michezo, 
kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.


 
1 Maoni