Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata
utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli
za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia),
Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce
Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa
Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza
kushoto.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu,
Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja
na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza
Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya
3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika
mwishoni mwa mwaka huu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Profesa Rwekaza Mukandara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa
ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli
hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga
tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi
katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mke wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana
Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi
wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika
kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za
wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga
mkono wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Taaswira
ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake
umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka
huu.PICHA NA IKULU.
0 Maoni