Unordered List


TANZANIA YA VIWANDA: MKOA WA SIMIYU KUZINDUA VIWANDA VIWILI JUMA HILI

SIMIYU YA R.C MTAKA YENYE VIWANDA YAWADIA 

Katika  hali ambayo watu wengi hawakutarajia ni Mkoa wa Simiyu kuanza uzalishaji wa viwanda vidogo vidogo.

Ndoto hii ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Ndg Antony Mtaka sasa Yaanza Kutimia.

Tarehe 11 mwezi Octoba Historia kwa wana Maswa na Meatu Mkoani Simiyu  itaandikwa  kwa Kiwanda cha Kwanza cha kusindika maziwa Mkoani Simiyu na Kiwanda Cha Utengenezaji wa Chaki  vitazinduliwa na Mhe Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama.

Hii ni kuendana na Kauli Mbiu ya Mkuu wa Mkoa isemayo "ONE DISTRICT ONE PRODUCT"

AkizungumzaMkuu wa Mkoa  Ndg Antony Mtaka aliwataka wana Meatu na Maswa Mkoani Simiyu kuunga Mkono jitihada hizo Kwa wananchi Kutunza na Kununua Kwa wingi Bidhaa zitakazo zalishwa na Viwanda Hivyo kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza Tatizo la Ajira Kwa Vijana Mkoani Simiyu.



Chapisha Maoni

0 Maoni