Jumatano, 19 Oktoba 2016

WAZIRI MAKAMBA AENDELEA NA ZIARA YA UKAGUZI WA MAZINGIRA MKOANI IRINGA


2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira January Makamba ameendelea na ziara mahsusi ya kutembelea, kutambua na kushughulikia changamoto zilizopo kwenye mazingira ambapo amemaliza mkoa wa Morogoro na kuanza mkoa wa Iringa.
Akiwa mkoani Iringa Waziri Makamba amepata wasaa wa kutembelea bwawa la Kuzalisha Umeme Kihansi na Maabara ya Chura wa Kihansi ambapo alipongeza juhudi za uhifadhi wa mazingira kuzunguka eneo hilo ambapo wanapatikana chura wa kipekee duniani na ambalo pia ni moja kati ya vyanzo tegemezi vya nishati nchini. Katika kutambua umuhimu wa eneo hilo Waziri Makamba ameahidi kuanza mchakato wa kutangazwa kwa eneo hilo kuwa eneo mahsusi ili kulilinda zaidi kisheria.
whatsapp-image-2016-10-18-at-4-11-13-pm
Waziri Makamba pia alifika katika Kijiji cha Mwatasi, Wilaya ya Kilolo ambapo alizungumza na wakazi wa Vijiji vya Mwatasi na Wangama pamoja na viongozi wa vijiji hivyo, ambapo amepongeza kazi kubwa inayofanywa na vijiji hivyo katika utunzaji wa vyanzo vya maji ambavyo vinapeleka maji katika Bwawa na Mto Kihansi pamoja na mto Kilombero. Katika kutambua mchango mkubwa wa kamati za Mazingira katika vijiji vya Mwatasi na Wangama Waziri amezipatia kamati za mazingira za vijiji hivyo shilingi laki moja kwa kila kijiji ili kukuza na kufufua mfuko wa mazingira na kusaidia kuendeleza shughuli za uhifadhi lakini pia amemwagiza Mkurugenzi kuweka utaratibu wa kubakiza sehemu ya tozo wanazotozwa waharibifu wa mazingira zinabaki katika kusaidia shughuli za Kamati za mazingira za vijiji huku akiwasisitiza viongozi wa kamati hizo kufungua akaunti benki ili fedha ziwekwe huko. Akiwa kijijini hapo pia Waziri alitembelea moja kati ya vyanzo vya maji na kuona watu wamelima mbogamboga na kupanda miti ndani ya chanzo. Waziri ameagiza Serikali ya Wilaya/Halmashauri/NEMC kuhakikisha kuwa ndani ya wiki nne watu hao wawe wameondolewa,miti iliyopandwa katika chanzo cha maji ikatwe na chanzo kirejeshwe katika hali yake.
whatsapp-image-2016-10-18-at-4-12-38-pm
Waziri Makamba pia amefika katika misitu ya kampuni ya New Forest (Lukosi plantation) kukagua shughuli zinazofanywa katika eneo hilo na kuona jinsi gani utunzaji wa mazingira unapewa kipaumbele na kuzingatiwa katika shughuli za kila siku za kampuni hiyo.
Uongozi wa Wilaya ya Kilolo ulitoa malalamiko juu ya kampuni hiyo Kampuni hiyo kuchelewa kulipa kodi na tozo stahiki kwa Halmashauri ya Wilaya. New Forest walisema wanaidai TANESCO ndio maana hawajalipa na Waziri Makamba amewaagiza walipe mara moja kwani kudai TANESCO sio sababu stahiki inayokubalika ya kutolipia kodi.
Waziri Makamba pia alifika katika mkoa wa Iringa na kupokea taarifa ya mazingira ya mkoa kabla ya kupata wasaa wa kufika katika kituo cha maji Ndiuka ambacho ndicho husafisha maji na kutibu maji toka mto mdogo Ruaha kabla ya kusambazwa kwa matumizi ya kila siku. Akiwa katika kituo hicho Waziri Makamba amepokea taarifa toka kwa Mkuu wa Mko wa Iringa Bi Amina Masenza juu ya uchafuzi wa Mazingira katika mto ambao ni chanzo kikuu cha maji kwa Manispaa ya Iringa ambapo alisema kwamba kuna watu wanachoma matofali kandokando ya mto na wengine wanachimba madini, Waziri ameagiza NEMC na Mamlaka za Manispaa na Jeshi la Polisi wapite kwenye kingo nzima za mto huo na kuwaondoa wachafuzi wote na kuwashtaki mara moja.
Vilevile Waziri ameupongeza mkoa wa Iringa kwa jitihada zake katika uhifadhi na utunzaji wa Mazingira ambapo taarifa ya mkoa imeonyesha kuwa kati ya mwaka 2012/2012 na 2015/2016 mkoa umefanikiwa kupanda miti takribani Milioni 60. Pia amepongeza juhudi za mkoa kutunza vyanzo vya maji ambapo kati ya vyanzo 2600 vilivyopo takribani vyanzo 1700 vimehifadhiwa.
whatsapp-image-2016-10-18-at-4-07-27-pm
Waziri Makamba ameahidi kuendelea kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali Kuu, Wizara na taasisi husika katika kuhakikisha mkoa wa Iringa ambao ni wa kipekee na kimkakati kimazingira unafanikiwa zaidi na zaidi katika uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.
whatsapp-image-2016-10-18-at-4-14-28-pm whatsapp-image-2016-10-18-at-4-14-27-pm whatsapp-image-2016-10-18-at-4-12-28-pm
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu