Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza kushoto,
akishuhudia Viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY nchini hapa
wakisoma ramani ya Tanzania katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini
Riyadh, ili kuifahamu vizuri Tanzania na maeneo watakayofikia katika
msafara wao wa kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma za
afya bure kwa siku 10 kwenye Hospitali za Chake Chake na Wete. Picha na
Mpiga Picha Wetu, Riyadh. Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akiwa na viongozi wa
Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY ambao walifika Ubalozini mjini
Riyadh kujitambulisha na kukamilisha taratibu za safari kuingia
Tanzania. Madaktari hao wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Novemba
11.
0 Maoni