Jumatatu, 28 Novemba 2016

MAKADA KUTOKA CHUO CHA VIONGOZI WATENDAJI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) WAFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM, LEO


Na Dotto Mwaibale

UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao  Tse-Tung.

Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.
Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

" Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba,  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema Chana.
Alisema wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi wa Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bao, (kulia) kwenye Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo. Bo ni Mkuu wa msafara wa Makada kutoka chuo hicho ambao wapo nchini kwa ajili ya ziara ya mafunzo. Wapili kushoto ni Mjumbe w NEC Temeke, Phares Magesa, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Pindi Chana, Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Tanga Dk. John Mndolwa
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (kushoto), akimuonyeska Ilani ya Uchaguzi 2015-20, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi wa Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bao, (kulia) kwenye Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi ilani hiyo ya uchaguzi.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi ilani ya CCM, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi wa Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bao, wakati wa mazungumzo yao kwenye Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Dar es Salaam
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chama, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe huo kutoka CPC China. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali.
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Tanga, Dk. John Mndolwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe huo wa China
 Kijana wa CPC kutoka China akisalimia kwa furaha na Kijana kutoka Makao Makuu ya CCM, wakati wa mazungumzo hayo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akimkabidhi zawadi ya kitenge, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi wa Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bao

 Jia Bao naye akimkabidhi Madabida zawadi ya picha aliyopigwa alipokuwa katika ziara ya Kichama nchini China hivi karibuni

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu