Jumamosi, 19 Novemba 2016

UVCCM Mfungishieni virago vyake Milya mwaka 2020


Na Mwandishi wetu, SimanjiroKaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka leo jioni amepokelewa kwa mbwembwe, vifijo na hoihoi alipowasili wilayani Simanjiro kuanza ziara ya siku tatu mkoani Manyara .

Amesema anaanza ziara yake huku akitamani muda wa uchaguzi ufike ili mbunge wa Simanjiro (CHADEMA) James Milya afugishwe virago vyake kwa ridhaa za wananchi muda muafaka utakapowadia.

Shaka alitoa matamshi hayo mara ya kupolewa katika makutano ya wilaya za Siha, Hai, Arumeru na Simanjiro njia panda ya KIA nje kidogo ya mji wa Moshi.

Alisema amefurahi kupata mapokezi mazuri yenye heshima huku akiwahimiza viongozi wa UVCCM kuhakikisha zama ya mbunge Milya inazikwa na kusahauliwa ifikapo mwaka 2020 na jimbo hilo kurejea tena mikononi mwa CCM.

"Naanza ziara hii nikiwa sina raha kuliona jimbo hili liko mikononi mwa upinzani, jamani tumekosea wapi, tumejichanganya vipi hata tukalipoteza , tafuteni sababu za msingi, jiulizeni maswali kisha mpate majibu "alieleza shaka.

Kaimu huyo katibu mkuu alipowasili wilayani hspa akilakiwa na baadhi ya viongozi wa jumuiya ya vijana ya ccm mkoa Manyara na wilaya ya Simanjiro

Viongozi waliomlaki ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Manyara Raphael Sumaye , Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Simanjoro Kiria Ole Laizer Katibu wilaya ya Somanjiro Bakari Mwacha , Kamanda wa vijana wilaya ya Somanjiro Daniel Mamasita wakiwemo na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Somanjiro.

Kesho mapema asubuhi Kaimu Katibu Mkuu anatazamiwa kuzungumza na baraza la wazee la ccm wilaya ya simanjoro pamoja wajumbe wa kamati utekelezaji na baraza kuu katika kikao cha ndani kitakachofanyika katika ofisi za ccm wilaya ya simanjiro kabla kuzindua jengo jipya la kisasa la lililojengwa na uvccm wilayani ya Simanjiro.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu