Jumapili, 18 Desemba 2016

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Ameanza ziara ya siku 8 katika mkoa wa Kagera ambapo atatembelea wilaya zote 8 za mkoa huo.


Katika wilaya ya Biharamulo Leo Kaimu Katibu Mkuu alifanya shughuli mbali mbali za kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama na jumuiya zake kama:

Alipokea taarifa ya wilaya ya Biharamulo kuhusu utekelezaji wa  kazi za Chama, jumuiya ya UVCCM na Serikali.
Alishiriki ujenzi wa nyumba ya maabara na walimu katika kijiji cha  Kaniha.

Alikagua mradi wa maji safi na salama na uchimbajiwa visima vya maji katika kijiji cha Nyantakaro
Alipata fursa ya kuzungumza na vijana na wananchi wa ujumla katika kijiji cha Nemba na kusikiliza kero, changamoto na maoni ya vijana na  wananchi hao.
Alishiriki na kufungua wa jengo la kisasa la ofisi ya CCM kata ya Kabindi.
Alikabidhi kadi 115  za CCM, vijana, wazazi na amekabidhi kadi 30 kwa wanachama wapya kutoka CHADEMA waliojiunga na CCM
Katika ziara hiyo amefuatana na viongozi kadhaa wa  Serikali Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Sasa Malunde, Mkurugenzi wa Halmashauri na maafisa waandamizi wa kada mbali mbali serikalini ambao walitakiwa kujibu mambo kadhaa yaliyokuwa yakijitokeza yanahusiana na utekelezaji wa ilani ya CCM na maendeleo kwa ujumla.
Wengine ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake ambapo kesho  ziara hiyo itaendelea wilaya ya Ngara.
*End*
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwasili na Kulakiwa na Viongozi Wa Chama na Serikali Mkoani Kagera katika kijiji cha Kahina Mpakani mwa Mkoa wa Geita nA Kagera
 aimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akisalimiana na Mhe:Mkuu Wa Wilaya ya Biharamulo Bi Saada Malinde
 Mhe:Mkuu Wa Wilaya ya Biharamulo Bi Saada Malinde akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika kikao cha ndani
 aimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC akielekea kukutana na Wana CCM Wilayani Biharamulo
 Mwenyekiti Wa UVCCM Yahya akizungumza  katika mkutano wa Diwani wa kata ya NEMBE na Wananchi
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Pamoja na mhe: DIWANI wa kwanza Kushoto akigawa kadi 115 Kwa wanachama Wa CCM UVCCM na WAZAZI Pia ameweza kukaribisha wanacha toka Chama cha CDM 30
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC Akinywa Maji mara Baada ya kukagua Mradi wa Maji katika kata ya NYANTANGARA
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na Wajasiliali wadogo wadogo katika kata ya NEMBA
 :Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizindua Ofisi ya Chama kata ya KABINDI Lililo gharimu shilingi Million 3
Wananchi wa Kata ya KABINDI wakisililiza kwa Makini mara baada ya kuzindua Jengo la ofisi ya chama katika kata Iyo
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu