Na Is-haka Omar, Zanzibar
MADIWANI wa Manispaa ya Mjini, wamempitisha Khatib Abdulrahman Khatib , kugombea nafasi ya umeya wa manispaa hiyo.
Uchaguzi
huo ulimpendekeza meya huyo na kumpitisha baada ya kupata kura 27 za
madiwani wote, hatua ambayo itamfanya kuwania nafasi hiyo katika
uchaguzi wa Meya kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Khatib
alipitishwa kuwania nafasi hiyo katika Mkutano uliofanyika Ukumbi wa
CCM Mkoa Mjini Amani Unguja ambapo mgombea huyo atachaguliwa kwa kuwa
hakuna chama kingine chenye Madiwani ukiachia CCM na inatarajiwa
atashika nafasi hiyo kwa mara ya pili. Kwa sasa Khatib ndie Meya wa
Manispaa ya Mjini.
Madiwani
hao pia walipitisha majina ya Naibu Meya ambaye ni Bimkubwa Said Sukwa
aliepata kura 15, akimshinda mpinzani wake , Saleh Fasihi Saleh aliepata
kura 12.
Kwa
mujibu wa miongozo ya uchaguzi huo Majina hayo ya Meya na Naibu Meya
yatapigiwa kura na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Mjini.
Kupitia
Uchaguzi huo nafasi nyingine zilipigiwa kura ni Mwenyekiti wa Madiwani
wa CCM katika manispaa hiyo na kupatikana Omar Mwalimu Juma , aliepata
kura 13 na nafasi ya Katibu wa Kamati ya Madiwani iliyochukuliwa na
Makame Khamis aliepata kura 27.
Mapema
Akifungua Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
aliwataka Madiwani hao kuwachagua viongozi makini na wenye sifa za
kujituma kiutendaji.
“
Endelelezeni utamaduni wa Chama Chetu katika kufanya uchaguzi huru na
wa haki ili kupata viongozi watakaoweza kusimamia shughuli za manispaa
yetu kwa ufanisi.
Pia
epukeni makundi na badala yake kuweni wamoja katika kufanya kazi za
maendeleo ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wenu katika Manispaa ya
Mjini.”, aliwasihi Vuai na kuongeza kuwa Manispaa ya Mjini ndiyo kioo
cha Mjini wa Zanzibar hivyo lazima pafanyike kazi ya ziada kuhakikisha
panakuwa safi na kung’ara muda wote kama ilivyo Miji mingine Duniani.
Naibu
Katibu Mkuu huyo aliwasisitiza Madiwani hao kuwa Chachu ya kuleta
maendeleo katika Wadi zao na kubuni miradi inayoendana na matakwa halisi
ya wananchi ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa
vitendo.
Akizungumza
na Gazeti hili mara baada ya Uchaguzi huo Meya Mteule wa Manispaa hiyo
Khatib Abdulrahman Khatib aliwashukru Madiwani hao kwa kumuamini na
kumpitisha tena ili aweze kuendelea kuongoza Manispaa hiyo kwa awamu ya
pili.
Aliahidi
kuendeleza mikakati ya kimaendeleo ndani ya Manispaa hiyo ikiwemo
kushirikiana na viongozi wengine na wananchi kwa ujumla kuhakikisha
Manispaa hiyo inakuwa na hadhi inayoendana na historia ya Zanzibar
kimataifa.
Aliwakumbusha
wananchi kudumisha usafi na utunzaji wa miundombinu mbali mbali iliyomo
katika Manispaa hiyo ili kuepuka kuingia katika mikono ya kisheria.
0 Maoni