Alhamisi, 8 Desemba 2016

KONGAMANO LA UVCCM WILAYANI BUSEGA LAINGIZA WANACHAMA WAPYA ZAIDI YA 200


Mjumbe wa Baraza kuu la uvccm Taifa ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa leo tarehe 7/12/2016 wakiwa wameambatana na Mkuu wa wilaya ya Busega ameshiriki katika kongamano lililoandaliwa na umoja wa vijana wa Wilaya ya Busenga na kutolewa mada mbalimbali.Katika mada zilizozungumzwa ni Suala la Maambukizi ya ukimwi, mada kuhusu Rushwa iliyotelewa na Afsa wa Takukuru, mada ya ujasiliamali imetolewa na afsa Vijana wa wilaya ya Busega na Mada inayohusu vijana na Siasa imetolewa na Mjumbe wa baraza kuu la uvccm  Taifa ndugu Rashid Gewa.

Baada ya hapo Mjumbe wa baraza kuu la uvccm Taifa ndugu Rashid Gewa akiambatana na DC wa Busega Mh Tano Mwera amegawa kadi kwa wanachama wapya zaidi ya mia mbili (200)   na baada ya hapo walipewa kiapo cha utii na kaimu katibu wa mkoa wa Simiyu ndugu Peter Masele Paul.Mjumbe huyo wa baraza kampongeza kijana mbunifu anayetengeza viatu kwa ubunifu wake mwenyewe na  kumpatia Shilingi laki moja aongezee kwenye mtaji wake.


Katika nasaha zake amewaasa vijana kufuata mambo makuu Sita yenye maadili katika umoja wa Vijana na ccm ambayo ni.Uadilifu, uwajibikaji, ubunifu,  ushirikiano, uwazi na matumizi sahihi ya rasilimali za umma.Pia amewaonya kuiepuka rushwa katika uchaguzi wa mwakani na kuwasihi vijana waliyozidi umri wa miaka 30 wasiombe kugombea tena katika umoja huo wa uvccm na kumuagiza katibu wa wilaya ya Busega kuzingatia kanuni na sheria za umoja huo ili kupisha wale wenye umri wa kuanzia miaka 14 -30 kupata nafasi na wengine wakajaze kwenye jumuiya zingine kama wazazi na UWT.Amesema atakuwa wa kwanza kuwapinga wale wote waliyozidi umri kuanzia matawi hadi Taifa.

Pamoja na yote kampongeza DC wa Busega ambaye ameonesha nia ya kusimamia  5% ya vijana kutoka halmashauri ya Busega kuwaendea vijana wote wa wilaya yake na kuwaomba wachangamkie furusa hiyo kwani DC ameonesha nia thabiti ya kuwainuwa vijana wote bila kujali vyama vyao kwa hilo alimshukuru sana Mh DC.

Mjumbe wa Baraza kuu la uvccm Taifa ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Ndg:Rashidi Gewa akizungumza na Vijana Wa Uvccm katika kongamano la Vijana Wilayani Busega
Mhe Mkuu Wa Wilaya ya Busega Mh Tano Mwera wa Kwanza Kulia akimvalisha kofia Kijana mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Uvccm
Mjumbe wa Baraza kuu la uvccm Taifa ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Ndg:Rashidi Gewa akimkabidhi kadi Binti Mwanachama mpya wa UVCCM
Wanachama Wapya Zaid ya 200 wakila kiapo mara Baada ya Kupokea kadi za Uwanachama na kujiunga rasmi na Uvccm
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu