Alhamisi, 22 Desemba 2016

SHAKA VIJANA FICHUENI WAHAMIAJI HARAMU.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akipokea Salaam za Shukrani Kwa niaba ya Rais  kwa mama MjaneAGRIPINA ANGERO ambaye alie jengewa Nyumba Mpya na Ya kisasa na Mhe : Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuri.

.................................................................................

 Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  tarehe 20 aliendelea na ziara yake mkoani Kagera wilayani KYERWA .Akiwa njiani kuelekea Wilayan Kielwa aliongozana pamoja na  viongozi   mbalimbali kumtembelea Mjane mama AGRIPINA ANGERO ambaye alie jengewa Nyumba Mpya na Ya kisasa na Mhe : Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuri mara baada ya nyumba aliokua akiishi mjane huyo kubomoka tokana na Tetemeko.

Akiwa hapo kaimu Katibu mkuu alipokea salamu za Shukrani kutoka kwa Mama Mjane AGRIPINA ANGERO  kwenda kwa mhe Rais kwa kumjali na kuguswa na Shida za wanyonge.Kaimu katibu mkuu amewaagiza UVCCM wilaya ya Karagwe ndani ya siku 3 kwenda kwenye eneo hilo kufanya Usafi  ili kumsaidia mama mjane. 

Pia akiwa Wilayani Karangwe kuelekea Wilayani Kielwa Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  alishiriki zoezi la kugawa vifaa vya ujenzi kwa familia 10 Wahanga wa Tetemeko vifaa hivyo vimetolewa na Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera usharika wa Karagwe akigawa vifaa hivyo kaimu katibu mkuu amelishukuru kanisa la Anglican kwa kuendelea kuguswa na maafa ya tetemeko.

Mara baada ya kupokelewa kijiji cha Changa akiwa kijijini hapo alipata fursa ya kukagua tenki la maji linalo tumiwa na wananchi katika kijiji hicho
Pia amepata fursa ya kutembelea mradi wa nyumba wa Uvccm tawi la Nkwenda akiwa hapo aliwataka vijana kuacha ulalamishi wajitume katika kazi za ujasiliamali na kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi.

Ukaguzi  Wa Utekelezaji wa ilani ulimfikisha Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  kuona pia ujenzi wa barabara ya Nkwenda-Mabira yenye urefu wa Km 31 iliyogharimu Tsh bil 2.

 Mara Baada ya zoezi hilo kaimu katibu mkuu alifika kijiji cha Kakanja sanjari na kutembelea mradi wa ufugaji nyuki akiwa hapo aliwapongeza wananchi kwa kuweza kuwekeza kwenye ufugaji nyuki na pia alitoa kadi kwa wanachama wapya 59 Uvccm na CCM.

Hatimaye Msafara wa kaimu katibu mkuu ulifika ofisi ya Mkuu wa wilaya Kyerwa Kanali mst Lissu kusomewa taarifa ya Serikali. na Mara Baada ya Kupokea Taarifa hiyo  alihudhuria baraza la Vijana wilaya akihutubia baraza hilo Kaimu katibu mkuu amewataka vijana kuacha kuwaficha wahamiaji haramu badala yake washirikiane na serikali katika kulinda mipaka na Wahamiaji haramu kutokana na wilaya kupakana na nchi za Rwanda na Uganda.
 Alisema"Hakikisheni mnawafichua wahamiaji haramu wote bila uoga hawa ni hatari kwa usalama wa nchi yetu" hali kadharika Tuache kupenda vya dezo kwa kuwafanya Vibarua katika Mashamba yetu ilhali tunajikaanga wenyewe pia'' Alisema Shaka.

Pia Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka ameitaka halmashauri wilaya Kielwa kuendelea kutoa mikopo kwa vijana  kwa kuzingatia 5%  ya mikopo ya vijana Wilayani humo Alisema'' Viongozi wa Halmashauri ifikie hatua Tuwajali Vijana kwa kuwapatia Mikopo ili waweze kujikwamua kiuchmi hawa ndio wapiga kura wetu Uvccm italala Mbele na Halmashauri itakayo kaidi Utoaji wa Fedha za Mikopo kwa Vijana''
Eneo la Nyumba ya Nyumba Mpya na Ya Mama MjaneAGRIPINA ANGERO  kisasa na Mhe: Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuri iliyopo katika Kijiji cha Kayanga Wilayani Karagwe.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa  Ndg:Shaka Hamdu Shaka wa Tatu Kulia akigawa Vifaa Vya Ujenzi Vilivyo tolewa kwa Hisani ya  Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera usharika wa Karagwe kwa Familia nane Maskini zilizo kubwa na Tetemeko.
  •  Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe  Godfrey Ayub  Mheluka Mwenye Suti Nyeusi akiagana na kaimu katibu Mkuu Shaka Mara baada ya Kumfikisha Wilayani Kielwa.

kaimu katibu Mkuu Shaka akikagua Ukaguzi  Wa Utekelezaji wa ilani  Wilayani Kielwa ulimfikisha Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  kuona pia ujenzi wa barabara ya Nkwenda-Mabira yenye urefu wa Km 31 iliyogharimu Tsh bil 2.

 Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akiambatana na Mkuu wa wilaya Kanal Mstaafu Shaaban Lissu  na Viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali  akikagua Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wiliya iliyopo katika kijiji cha Rubwera Kagenyi Wilayani Kielwa.
  Mkuu wa wilaya Kyerwa Kanal Mstaafu Shaaban Lissu  akimsomea Kaimu katibu Mkuu Taarifa ya Serikali juu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020.
Mwenyekiti wa Uvccm Yahya Kateme akimkaribisha Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Kuzungumza na Baraza la Vijana Wilayani Kielwa.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Kielwa.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akigawa kadi kwa Mmoja kati ya Wanachama  Wapya 173 Wilayani Kielwa Mkoa wa Kagera
Wanachama wapya wakila Kiapo na Yamini ya Chama Mara baada ya kupokea kadi ikiwa ni Ishara ya Kujiunga Rasmi na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu