Jumapili, 11 Desemba 2016

TCRA WACHUKULIENI HATUA WANAOJIITA SAUTI YA KISONGE.


Hivi karibuni kumeibuka page moja Facebook iliyojivika jina la "SAUTI YA KISONGE"

Page hii imekuwa ikizusha mambo mbalimbali yasiyo na ukweli wowote ule na kusababisha kuzua Taharuki ndani ya jamii.

Mfano wa uzushi wao ni hii leo tarehe 11 Desemba 2016  wamepost Picha ya Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Taifa ndg SHAKA HAMDU SHAKA ikiwa na Maneno Eti amemuonya Waziri wa Ardhi ndg WILLIAM LUKUVI kuhusiana na masuala ya Ardhi.

Na wamediriki kuweka picha na kusema anafafanua vifungu vya katiba.ukitazama picha hiyo ni barua yenye Nembo ya UVCCM sasa sijui katiba siku hizi inakuwa na nembo ya Uvccm?

Walichofanya ni kuchukua picha ya mwezi Julai na kudanganyia eti kikao cha Leo.

Ukweli ni Kwamba chama cha mapinduzi na Jumuiya zake viongozi wake sio Mapoyoyo wa kupiga makelele.

Na hakuna Mgogoro wa Ardhi kama inavyosambazwa na Wafuasi wa CUF KUPITIA HII PAGE FEKI YA SAUTI YA KISONGE.

VIJANA WA CCM wamefundwa na kulelewa katika maadili mema sio waropokaji na makasuku.

Kitendo cha kumsingizia Kaimu katibu Mkuu Uvccm Taifa kuwa Ametoa kauli na ilihali hajawahi kuzungumzia lolote ni UPUUZI mkubwa.

Tunaitaka TCRA  ichukue hatua dhidi ys watu wanaopika maneno na kuchonganisha.

Wanaofanya vitendo hivi wapo na wanajulikana wachukuliwe hatua za kisheria kupitia Sheria ya Mitandao ya Mwaka 2015.

  Uvccm inatoa onyo kwa wahusika kuacha mara moja tabia hii ya kutafuta umaarufu kupitia migongo ya watu na kutumia nembo ya jumuiya yetu kinyume na utaratibu wa kikanuni na  kisheria.

SIASA SIO UKASUKU NA KUTUNGA MANENO bali ni mipango ns Sera imara zinazokubalika kwa wananchi na sio uzushi.

IMETOLEWA NA:

CHIEF SYLVESTER YAREDI

KAIMU MKUU WA IDARA UHAMASISHAJI SERA UTAFITI NA MAWASILIANO UVCCM TAIFA

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu