• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Alhamisi, 26 Oktoba 2017

SHAKA:AWATAKA WAGOMBEA UVCCM KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA UCHAGUZI.

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA WOTE WALIOOMBA KUTEULIWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI NGAZI YA MIKOA NA TAIFA

Kwa Wana Jumuiya wote hususan wale wote walioomba kuteuliwa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye UVCCM ngazi ya Mikoa na Taifa. Kila mmoja anapaswa kuusoma, kujilinda, kuzingatia, kuufahamu na kuuelewa ujumbe huu muhimu.

Zipo taarifa za uhakika zenye vielelezo vyenye ushahidi kuwa baadhi ya walioomba nafasi za kuteuliwa kugombea ndani ya UVCCM, wameanza kuitisha vikao vya mizengwe na kufanya kampeni za chini kwa chini kinyume na Kanuni, Taratibu  na mwenendo wetu wa Uchaguzi.

Ukusanyaji wajumbe kwa maana ya wapiga kura katika eneo ambalo si halali kikanuni na kiutaratibu linatoa tafsiri na kujenga  mazingira ya rushwa pia ukiukaji na uvunjaji wa kanuni  za Uchaguzi za Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.  

Ifahamike kuwa uchaguzi huongozwa na Katiba, Kanuni, Taratibu, miongozo na maadili halali hivyo kila mgombea anapaswa kuheshimu taratibu hizo, sambamba na kuheshimu miiko ya uchaguzi. 

Hadi sasa hakuna mwombaji wa nafasi yoyote aidha wa nafasi ya Mkoa au Taifa aliyeteuliwa jina lake na kuwa mgombea halali. Mamlaka za uteuzi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni hazijatangaza majina ya wagombea walioteuliwa kutoka miongoni mwa waomba nafasi waliojaza fomu ndani ya UVCCM.

Ni kosa na marufuku Kikanuni na Kikatiba kwa muomba nafasi yeyote kuanza kupitapita Wilayani, Mikoani, mitaani, vichochoroni, kuitisha vikao haramu vya kampeni , kujinadi na kujieleza kabla ya ukamilishaji wa mchakato wa uteuzi na majina  kutangazwa.

Vitendo vyovyote vitakavyofanywa namuombaji wa nafasi aidha kwa kujinadi kwa kuitisha vikao haramu,  kujielezea, kutaja malengo au kuwashawishi wapiga  kura kwa njia ambayo si ya kidemokrasia ni kinyume na taratibu. Ushahidi ukipatikana na  kuthibitika kunaweza kukuondolea sifa ya kuteuliwa katika nafasi uliyoomba.

Tunaendelea kukumbusha kuwa hatutasita kumchukulia hatua za kimaadili mpambe wa muomba nafasi yoyote atakayebainika anakwenda kinyume na maelekezo haya pamoja na matakwa ya Katiba ya Chama Chama Mapinduzi na Kanuni za UVCCM.

Hata baada ya vikao vya uteuzi kukamilika mwongozo utatolewa kwa ngazi ya Mkoa hadi Taifa namna ya kufanikisha chaguzi hizo.

Chama Cha Mapinduzi ni baba na kinara wa demokrasia Tanzania, Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla, chaguzi hizi zinazoendelea ndani ya Chama na Jumuiya zake ni kielelezo tosha cha ukomavu wa demokrasia na kioo kinachoakisi heshima ya Chama na Jumuiya ndani na nje hasa katika kusimamia mambo yake ya msingi ya Kikatiba na Kikanuni.

Naendelea kuwakumbusha Vijana wote kuendelea kuishi katika maneno ya Usia ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli aliyowahi kutuasa wakati chaguzi hizi zikiendelea nanukuu

Natambua mnaendelea na Uchaguzi ni lazima kuheshimu Katiba ya Chama chetu na Kanuni zetu katika mchakato wa kuwapata Viongozi tutakaowapa dhamana. Vijana lazima wachague Viongozi wazuri, wazalendo, waadilifu, wachapa kazi watakaolinda maslahi ya CCM na UVCCM  na si maslahi binafsi kataeni na kupiga vita rushwa kwa nguvu zote na watakaobainika kutoa au kupokea rushwa hatua za haraka zichukuliwe”; Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

Nachukua nafasi hii kwa sauti ya juu kabisa kuwaonya, kuwaasa, kuwakanya na kuwazuia wale wote ambao aidha wanafanya kwa makusudi au kujisahau waelewe kuwa Kanuni ya Uchaguzi iko pale pale na itatenda haki kama msumeno. Vile vile watambue kuwa tunawamulika na kuwafuatilia nyendo zao zote na ikibainika, taarifa zao zitawasilishwa katika vikao kwa hatua zaidi za Kimaadili.

Ahsanteni 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU
Share:

Jumamosi, 21 Oktoba 2017

VIJANA WAZALENDO WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI MJINI DODOMA LEO.

Mhe Jordan Rugimbana Mkuu wa mkoa wa Dodoma akikabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka Taarifa ya  Tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi lilifanyia mkoani Dodoma
Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka ( MNEC ) akitoa Tamko la Vijana wazalendo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
Mhe Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana ajira na Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza na Vijana wazalendo  katika
Hafla fupi ya Kukabidhi tamko  la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi Mjini dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana akizungumza na Vijana wazalendo mara baada ya  kupokea taarifa ya Tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi

baadhi ya mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali za kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kulinda Rasilimali Za Nchi. ( Picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
Vijana wakiwa katika burudani.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
Vijana wakiwa katika burudani.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )

Share:

Alhamisi, 12 Oktoba 2017

SHAKA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIET YA BARAZA KUU UVCCM TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM


Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vitajadili waombaji wa nafasi mbali mbali za uongozi kwa nafasi za Mkoa na Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kabla kuwasilisha katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi kwa uteuzi wa mwisho.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )
Share:

KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA(TIC) YAKANUSHA TAARIFA YA ILIYOTOLEWA NA GAZETI YA FINANCIAL TIMES KUWA SERA ZA UWEKEZAJI TANZANIA ZINAKIMBIZA WAWEKEZAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Ndg. Geoffrey Mwambe amesema kwamba taarifa zilizotolewa na Mwandishi wa FT. John Aglionby kuhusu mazingira ya Uwekezaji Tanzania kuwa yanatishia wawekezaji si sahihi na yanalenga kupotosha ukweli kuhusu hali halisi kuhusu Uwekezaji Tanzania.

Mwandishi huyo wa Financial Times ametoa maelezo ambayo amesema yametolewa na Muwekezaji Aliko Dangote maelezo ambayo yamelenga kusukuma Agenda yake ambayo haijulikani na yenye lengo la kupotosha sera za uwekezaji na kuwaogopesha wawekezaji ambao wameendelea kuiamini Tanzania na kuwekeza mitaji yao mikubwa hapa nchini.

Hatuamini kuwa Ndugu Dangote anaweza kuwa msemaji wa kuhusiana na sekta ya madini kwa hapa nchini. Amewekeza kwenye sekta ya viwanda na serikali imekuwa mstari wa mbele kusikiliza na kuyafanyia kazi maoni ya mfanyabiashara huyo ili kuweza kuboresha mazingira yetu ya uwekezaji hapa nchini. Serikali yetu imejidhatiti katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na imedhamiria kuhakisha uwekezaji huo unakuwa na faida kwa watanzania nan chi kwa ujumla.

Tunaamini kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha maelezo yanakuwa na pande mbili ili kuondoa utata utaojitokeza wa maelezo ambayo yanaweza kuathiri na kusababisha utata kwa wafanyabiashara walioiamini Tanzania kama sehemu yao ya kufanya uwekezaji. Tanzania inathamini na kujali wawekezaji wa aina ya ya Aliko Dangote na mara nyingi tumekuwa tukiwasikiliza na kufanyia kazi maoni yao ili kurekebisha sera ili ziweze kuwa na manufaa kwa wote yaani waTanzania na wawekezaji. Kuna sera pamoja na sheria ambazo tumezifanyia marekebisho ili ziweze kuwa na manufaa kwa wote.

Hivi karibuni ni vizuri kufahamu kwamba DIL ilikuwa na matatizo mbalimbali na serikali iliweza kukaa na Dangote na kusikiliza matatizo yao na kutatua changamoto kadhaa zilizokuwa zinakwamisha uzalishaji katika kiwanda chake cha Saruji na kufikia muafaka wa kutatua matatizo yote ambayo kiwanda ilikuwa ina TIC pia imeanzisha juhudi maalum za kuhakisha kuwa huduma zinotolewa kwa wawekezaji zinaboreshwa ili kuweza kurahisisha utoaji wa huduma kwa ufanisi na kwa haraka. Kituo kimeweza kuanzisha Kamati Maalum ya Kitaifa ya Kuhudumia wawekezaji yaani NIFC ambapo matokeo makubwa yameweza kuonekana kutokana na uboreshwaji wa huduma zetu chini ya mahali pamoja .

Tunamshukuru sana Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za dhati za kupambana na rushwa juhudi ambazo zimeweza kuleta mafanikio n ahata kuifanya Tanzania kutajwa na ripoti mbalimbali za dunia kama mahala bora Zaidi pa kuwekeza Afrika. Zaidi ya ripoti tano zimeweza kuitaja Tanzania kwa mwaka huu pekee kama sehemu bora Zaidi ya mazingira ya uwekezaji Afrika. Tunajivunia juhudi kubwa sana alizozionyesha Rais wetu Mh.John Pombe Magufuli katika kuvutia uwekezaji nchini hasahasa katika kutokomeza rushwa, jambo ambalo mwandishi wa makala hiyo kwa sababu zake binafsi ameshindwa kuziweka bayana.

Ni muhimu sana kuelewa kuwa suala la kuwa na sera nzuri za uwekezaji kwa manufaa ya mwekezaji na nchi limepewa kipaumbele kikubwa na Serikali ya Awamu ya Tano. Tunahitaji sekta binafsi kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria na taratibu, mfano kulipa kodi stahiki wakati Serikali kwa upande wake ikiendelea kuboresha zaidi mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Katika makala yaliyotolewa na FT imejionyesha waziwazi kuwa mwandishi hafahamu vizuri Sheri ya Uwekezaji ya Mwaka 1997.

Sheria za Tanzania zinatambua umiliki binafsi wa mali na kuzuia uwezekano wa kutaifisha mali hizo bila sababu za msingi za kisheria. Vilevile Tanzania ni mjumbe wa Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) ambapo makubaliano ya wajumbe ni kutoruhusu utaifishwaji wa mali za uwekezaji pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID).

Tanzania inaendelea kuhamasisha uwekezaji nchini na Kituo cha Uwekezaji kimekuwa mstari wa mbele katika kushawishi wawekezaji na mashirika makubwa ya kimataifa ambayo tayari yana uwekezaji nchini kuongeza mitaji yao. Tanzania imeendelea kupokea wawekezaji wengi ambapo uwekezaji huo umesaidia katika kukuza uchumi katika Nyanja mabilimbali mfano kuzalisha ajira mpya na kuongeza mapato ya kikodi. Matokeo haya chanya yanatokana na juhudi za Serikali kujenga mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC amewashukuru wawekezaji waliowekeza mitaji yao Tanzania kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea na juhudi zake za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo mzima wa kuwahudumia wawekezaji.

Ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendela kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji, Serikali imeipa kipaumbele utekelezaji wa miradi ya miundombinu wezeshi ili kusaidia katika kupunguza gharama za uwekezaji. Baadhi ya miradi hii ni pamoja na Mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge, ujenzi wa barabara, ukarabati wa miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam (Gati 1-7), ujenzi wa Reli ya Kati kwa iwango cha standard gauge. Jitihada nyingine zilizofanyika hivi karibuni ni uanzishwaji wa Mfuko wa Benki ya Ardhi (Land Bank Fund) na kuboresha mfumo wa asajili wa makampuni BRELA.

Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwenye kuvutia uwekezaji ukilinganisha na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki. “Tanzania imo katika orodha ya nchi kumi bora Afrika zinazovutia uwekezaji kulingana na ripoti ya Rand Merchant Bank (RMB). Vilevile Tanzania imeendelea kuwa na kiasi kikubwa cha mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya nchi (foreign direct investment) ukilinganisha na nchi nyingine za Jumuiya ya Africa Mashariki” amesema Bw.Mwambe
Share:

Jumatano, 27 Septemba 2017

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu,wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.

 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndg. Phili Mangula akikaribishwa ukumbini katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe  Magufuli akiwasili ukumbini kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na nyuma ya Makamu  wa Rais ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza wa Wakilishi la Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar ss Salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Rodrick Mpogolo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share:

Ijumaa, 22 Septemba 2017

HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI ILIOANDALIWA NA KINANA KWA AJILI YA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM MJINI DODOMA JANA SEPTEMBER 21,2017.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa akimtolea ufafanuzi wa zawadi ya kinyango Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam uku katibu Mkuu wa (CCM) akishuhudia zoezi hilo,wakati wa hafla ya Chakula cha Jion ilioandaliwa na kinana.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza kabla ya Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam kukabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa wakati wa hafla ya Chakula cha Jion.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza na balozi wa Vietnam Nguyen kim Doanh.


 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akifurahia jambo na wageni wake toka chama cha Kikomunisti cha Vietnam (VCP) jana wakati wa hafla ya chakula cha jion.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jion.
 Wajumbe wa Chama cha kikomunisti cha Vietnam (VCP) pamoja na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazaza CCM wa (pili toka kushoto) wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
Baadhi Wajumbe wa Sekretariet wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
 Katibu Mkuu wa CCM Comred Abdurahman Kinana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Juma Kimbisa pamoja na Katibu wa idara ya SUKI kanal mstaaf Ngemela Rubiga wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion  Katibu mkuu wa CCM alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar DKT.Abdallah Mabodi akiagana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika hafla ya chakula cha Usiku ilioandaliwa na Katibu mkuu wa CCM Comred Abdulrahman kinana Mjini dodoma.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comred Abdulrahman Kinana akiagana na Mgeni wake Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha jion aliomwandalia mgeni wake   Mjini dodoma. (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)Share:

Jumapili, 10 Septemba 2017

SHAKA AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA NYUMBANI KWAKE MJINI DODOMA.

Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akizungumza na Kaimu Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka (kushoto) wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma

Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwonyesha kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka kinyango chenye uzito wa tani 1 wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliochorwa na Mwanafinzi wa darasa la saba Mwaka 1982 wakati wa hali ngumu ya uchumi nchini.
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliyochorwa na mjuu wake ikimuonesha yeye na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 Picha ya pamoja Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela na Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha
 kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka  akimuaga  Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela alipomtembelea nyumbani kwake Mtaa wa Kilimani Mjini Dodoma(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)


.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM