*WASITUMIE UONGO NA SHIDA ZA WATU KUSAKA UMAARUFU WA KISIASA
Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimewasihi viongozi wa vyama vya wapinzani kujikita
katika siasa safi na uongozi bora, kwa kuachana na matamko ya uongo
yanayosababisha taharuki katika nchi na kuchonganisha wananchi na
serikali yao, kwa kuwa vitendo hivyo havina manufaa kwa mustakabali wa
maendeleo ya taifa.
Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Huphrey Polepole,
wakati akizungumza na waandishi wa habari, leo Januari 17, 2017, katika
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, kutoa
ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kichama.
Polepole amsema, wapinzania wamekuwa wakitumia matatizo ya wananchi na
kutoa matamko ya uongo ili kutia nchi katika taharuki kwa lengo la
kujitafufia umaarufu wa siasa vitendo ambavyo alisema, havisaidii
wananchi wala wanasiasa wa vyama hivyo katika kuleta maendeleo ya nchi.
Alisema, mbali na matamko ya viongozi wa vyama hivyo kutosaidia, katika
ujenzi wa maendeleo yamaendeleo ya nchijambo ambalo alisema za kueneza
maneno ya yasiyofanyiwa utafiti kwa lengo la kusababisha taharuki kwa
wananchi, jambo ambalo alisema, si miongoni mwa siasa safi wala uongozi
bora.
Polepole alisema, wapinzani wamekuwa wakifanya siasa za aina hiyo wakiwa
wanajua ubaya wake, kwa kuwa wao lengo lao ni kujaribu kuchonganisha
wananchi na serikali hata pale ambapo serikali inaonyesha juhudi za
dhali za kuijenga Nchi yenye uchumi imara wa viwanda.
"Nawaonba Watanzania tuwapuuze wanasiasa wa vyama hivi, tuendelee
kuiunga mkono serikali, ili itimize mipango na malengo iliyoweka,
ikiwemo kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kwa kuwa nchi ya viwanda,
hali ambayo itasaidia sana kutukwamua Watanzania kutoka katika
umasikini", alisema Polepole.
Polepole alitaja kuwa miongozi mwa mambo ambayo katika kipindi hiki
wanayatumia kupotosha ili kujaribu kuletea taharuki wananchi ni pamoja
na kueneza propaganda kuwa Tanzania imekumbwa na baa la njaa na pia
kutumia matatizo waliyopata wananchi wakati wa janga la tetemeko la
ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera kama mtaji wao kisiasa.
"Kwanza mjue, kutungaza taarifa ambazo zitaleta taharuki katika jamii ni
kosa la jinai, lakini pia inajulikana na wenyewe wanajua, kwamba
Duniani kote zipo taratibu ya utangazaji wa majanga katika nchi yoyote.
Baa la njaa ni janga kubwa linapofikia kiwango kibaya, mwenye mamlaka ya
kutangaza ni Mkuu wa nchi", alisema Polepole na kuongeza;
Alisema, Tanzania haijawahi kupata njaa yenye kiwango cha kuitwa baa la
njaa, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hivyo wanaojaribu
kutangaza kuwa Nchi ipo katika baa la njaa ni kushindwa kufanya siasa
safi na kukosa uongozi bora kama ilivyo CCM ambayo mambo hayo inayo.
"Ingawa tumekuwa na tatizo la njaa katika sehemu chache za na kuwepo
upungufu wa mvua katika maeneo kadhaa ya nchi hali ambayo inaweza
kusababisha upungufu wa chakula katika maeneo husika, bado hili siyo baa
la njaa. Na kwa kuwa hili serikali inalijua inaendelea kuweka mazingira
mazuri ili kuweza kupelekwa vyakula maeneo yote kuondoa uhaba, na
kipindi hiki hatujafikia huko", alisema Polepole.
"Baada ya kuona hali ipo hivi nilitarajia viongozi wote bila kujali
vyama , tuhimize wananchi kutumia chakula vizuri wasikitumie katika
mambo ya anasa au kukiuza hovyo, lakini wao wanakimbilia kutangaza baa
la njaa wakati njaa yenyewe haijatokea, hawa watu wa ajabu sana',
alisema Polepole.
Alisema, kila kiongozi anayeongozwa na misingi ya uongozi bora na
mzalendo kwa nchi yake, analo jukumu la kuwahamasisha wananchi kutunza
vyakula walivyonavyo.
Kuhusu tetemeko lilitokea Bukoba na kusababisha uharibifu na vyumba za
watu na miundombinu mbalimbali alisema kama ilivyo ulimwenguni kote,
inapotokea mambo haya ya majanga serikali hujenga uwezo wake kwanza ili
kusaidia wananchi wake.
"Baada ya tetemeko lile, Serikali ilichofanya ni kujengea uwezo wa
wananchi wasiwe mbali na huduma ndiyo maana ikaimarisha miundombinu ya
elimu, afya na barabara, kwa sababu watu waendelee kupata huduma".
alimalizia Polepole
0 Maoni