Unordered List


UZINDUZI WA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA KUZALIWA KWA CCM..KONGAMANO LAFANYIKA SHINYANGA


Jumamosi Januari 28,2017- Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini katika mkoa wa Shinyanga kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM tarehe 05.02.1977.
…………………………………………………………………..
Kongamano hilo limefanyika leo Katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga,makada wa CCM na vyama vya upinzani na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo wanafunzi wa Shule ya sekondari Buluba na Kom sekondari.
 
Mada mbalimbali zilitolewa wakati wa kongamano hilo ikiwemo historia ya CCM na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
 
Katika kuadhimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM,Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga kitashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya matawi ikiwemo,kupanda miti,kusalimia wagonjwa,watoto yatima,walemavu,kutembelea shule,michezo na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.
 
Vyama asili vilivyozaa CCM ni Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika  na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar vyote vikiwa ni vyama vya ukombozi.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ni “CCM Mpya,Tanzania Mpya”.
 
Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa Kongamano hilo,ametusogezea picha 40 za matukio yaliyojiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga wakiwa meza kuu.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura,akifuatiwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya,Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid na meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehekea miaka 40 ya CCM watashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo sambamba na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara
Makada wa CCM na wazee wa CCM wakiwa ukumbini
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura alisema lengo la maadhimisho miaka 40 ya CCM ni kujimbusha walipotoka,walipo na wanapoelekea.Kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rajab Makuburi
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza ukumbini
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akifungua kongamano hilo ambapo aliwataka wanaCCM kujivunia mafanikio ambayo yamepatikana tangu chama hicho kianzishwe mwaka 1977
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akisitiza jambo ukumbini
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wanachama wa chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla kuendeleza mshikamano uliopo nchini
Wanafunzi wa shule ya sekondari KOM wakiwa na mwalimu wao ukumbini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa ukumbini
Wafuasi wa CCM wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Mwalimu Patrick Kija alitoa mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi na kuelezea harakati za ukombozi kutoka enzi za ukoloni
Mwalimu Patrick Kija akitoa historia ya CCM
Tunamfuatilia mtoa mada…
Aliyekuwa katibu tawala wa CCM mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akichangia mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM tangu kianzishwe mpaka sasa.Alisema hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeimarika zaidi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa na diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole wakifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe alisema chama hicho kimeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya ,uchumi n.k
Tunafuatilia kinachoendelea
Meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akionesha ilani ya uchaguzi ya 2015 ya CCM wakati akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM katika awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli.
Mwendapole aliwataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaobeza mafanikio yaliyofikiwa na CCM 
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Makada wa CCM na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea….
Mwanachama wa CCM Joseph Maige akichangia hoja ukumbini
Viongozi wa CCM wakifuatilia michango ya washiriki wa kongamano hilo
Kada wa CCM Charles Gishuli akichangia mada ukumbini
Mkuu wa wilaya mstaafu Zipporah Pangani akichangia hoja wakati wa kongamano hilo ambapo aliomba Chama Cha Mapinduzi kijikite katika kutoa elimu juu ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho sambamba na kuimarisha chama katika ngazi ya matawi
Mwanafunzi Mariam Mrisho anayesoma kidato cha tano katika shule ya sekondari Buluba iliyopo mjini Shinyanga akichangia hoja katika kongamano hilo
Kada wa CCM Mussa Jonas akichangia hoja ambapo alisisitiza umuhimu wa Chama Kujulikana kwanza badala ya mtu kujulikana zaidi
Mwanafunzi Stephen William kutoka Kom sekondari akizungumza ukumbini
Vijana wa CCM wakipiga makofi baada ya kufurahia jambo ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Kanali Mstaafu Tajiri Maulid akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehea miaka 40 ya CCM wamejipanga kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini akizungumza ukumbini
Mwenyekiti wa CCM mko wa Shinyanga Erasto Kwilasa akifunga kongamano hilo ambapo aliwasititiza wanachama wa CCM kutoendekeza makundi ndani ya chama
Kwilasa alisema pia alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kwa kujali wanyonge na kuahidi kuwa chama hicho kitaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais Maguful katika kurudisha heshima ya nchi
Vijana wa CCM wakiondoka ukumbini

Chapisha Maoni

0 Maoni