Unordered List


KATIBU MKUU WA CCM KINANA KUONGOZA MAZISHI YA WANA CCM WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI KILIMANJARO..RATIBA HII HAPA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameondoka Dodoma kwenda mkoani Kilimanjaro kuongoza mazishi ya viongozi na wanachama wa CCM waliofariki juzi kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya CCM..

Kinana amesema atashiriki mazishi hayo ambayo yatafanyika kwa siku tatu tofauti.
Kulingana na taratibu ilizopatiwa ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM kutoka CCM mkoa wa Kilimanjaro, Mjumbe wa NEC wilaya ya Same, marehem Ally Mbaga atazikwa Usangi, Mwanga kesho tarehe 08.02. 2017 saa 9.00 alasiri.

Mwenyekiti wa UVCCM Hai, Anold Swai, atazikwa Masama Mashariki katika kijiji cha Mbweera tarehe. 10.02.2017 kuanzia saa 8 mchana.

Mwanachama wa CCM Edwin Msele atazikwa eneo la Ukaoni Moshi Vijijini tarehe 11.02.2017 saa 9.00 alasiri. na mwanachama mwingine Anastazia Mslamsha, ataagwa alhamis tarehe 09.02.2017 kuanzia asubuhi kwenye Chuo Cha Ushirika Moshi na kuzikwa Rombo siku hiyo hiyo alasiri.

Chapisha Maoni

0 Maoni