• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ijumaa, 31 Machi 2017

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM) KWA VYOMBO VYA HABARI UPANGA DAR ES SALAM IJUMAA 31 MACHI 2017


  VMM/U.80/8/Vol.I59                          31/03/2017

TAARIFA YA  UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM) KWA VYOMBO VYA HABARI UPANGA DAR ES SALAM  IJUMAA 31 MACHI 2017

Ndugu waandishi wa habari,

Tunawashukuru kwa kupokea wito wetu na  kuja, karibuni sana tunawaahidi kwamba  tutaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua.

Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unavipongeza sana vyombo vyote vya habari nchini kwa juhudi zenu za kuhabarisha, kuelimisha, kuwaasa, kuwaelekeza na kuihabarisha jamiii katika masuala kadhaa yanayohusiana na mipango ya maendeleo,   mikakati, sera na malengo ya Serikali  na mipango ya vyama vya siasa.

Ndugu Waandishi wa habari.

Tumewaita leo kuzungumzia mambo 2 makubwa, na suala zima la mtikisiko wa demokrasia katika  mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika Bunge la Jumuiya ya  Afrika Mashariki  (EAC) ulivyoendeshwa ndani ya vyama vya upinzani  nchini.

Bunge la Afrika Mashariki kama mjuavyo ni chombo kikubwa na chenye heshima ya pekee katika kanda yetu. Kuwepo kwake kunaashiria muendelezo wa kufufua dhana, dhamira, mikakati, fikra na malengo ambayo yaliasisiwa na waasisi wa Mataifa yote yaliyomo  katika Kanda yetu ili hatimaye siku moja ishuhudiwe Kanda hii na Bara zima la Afrika likiunda dola moja.

Ni jambo la heri na faraja kuona EAC  ya  sasa ikiwa ni yenye kufikia malengo ya  utengamano na mafanikio hususan katika nyanja za kiuchumi na kiusalama kama vile  kuwa na  Pasi moja ya kusafria, miingiliano ya wananchi wake katika ufanyaji wa biashara pia mkakati kuelekea kupata  viwango sawia vya ushuru wa Forodha.

Masuala mengine ni kuona  maeneo ya mipaka yetu kukiendelea kuwa na ustawi wa hali ya utulivu na usalama, wakati huo EAC ikifanya kila linalowezekana kumaliza migogoro yake ya kisiasa ambapo mazungumzo ya upatanishi huko Burundi yamekuwa yakiendelea  chini ya mpatanishi mkuu  Rais mstaafu Benjamin Mkapa sambamba na wananchi wa pande zote za nchi wanachama tukishuhudia  wakiishi kwa maelewano, umoja, udugu na mafahamiano.

Ni katika jumla ya mambo yanayofurahisha na pengine yakiwasuta na kuwaaibisha maadui na vibaraka ambao aghalab  hutumiwa kwa malipo yenye ujira wa dhambi  toka kwa mabeberu katika kuhakikisha  mipango batili ya kutaka kudhoofisha, kuigawa na kukwamisha juhudi za EAC isiimarike..

Aidha kuibuliwa na kupokewa kwa mpango uitwao " One Stop Boarder" yaani (OSB)  sasa umefanikiwa huko mipakani baina ya nchi wanachama.  Pia kuanzishwa  miradi mikubwa ya kiuchumi mfano bomba la mafuta toka Kampala (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) ujenzi wa reli toka kigali hadi Uganda huku EAC ikielekea kuwa na sarafu moja kabla ya kufikiwa azimio la  uundwaji wa Shirikisho moja.

Umoja wa Vijana wa CCM tumelazimika kuyataja na kuyaainisha maeneo hayo yaliopata mafanikio kwa uchache  lengo likiwa ni kuonyesha  uwepo na ustawi wa EAC pamoja na umuhimu wa bunge lake kama ni jambo nyeti na wala si suala dogo au la mchezo mchezo kama ambavyo baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeonyesha udhaifu.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeshindwa hata  kuteua wagombea ubunge wengi ili kuwania nafasi katika bunge hilo  la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu zinazotokana  aidha na ubinafsi, umimi na udikteta.

Tunachukua fursa hii kwanza kukipongeza Chama Cha Mapinduzi na wanachama wake wote 450 ambao kwa ujasiri, uwezo na kujiamini kwao wamethubutu kujitokeza na kuchukua fomu za  kuwania nafasi za ubunge wa EAC.

Kitendo cha wanachama hao wa CCM kujitokeza kwa wingi kimsingi  kimeidhihirishia dunia kwamba chama chetu bado ni cha kidemokrasia kinachoungwa mkono na kuaminiwa na wananchi wengi wakiwemo  Vijana, wanawake na wana taaluma mbali mbali wakitambua ndicho chama pekee imara chenye kujali, kuthamini na kufuata misingi ya usawa na demokrasia ya kweli.

Wanachama 450 wa CCM walichukua fomu kwa kufuata taratibu baada ya mchujo wa kidemokrasia kufanyika ndani ya CCM,  wanachama   12 wamebahatika kuteuliwa na vikao vya kikatiba  ambapo sasa wagombea hao watasimama mbele ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaka ridhaa  kwa kujieleza na kuomba kura.

Ndugu Waandishi wa habari,

Umoja wa Vijana CCM  kwa  tunasikitishwa sana na mwenendo wa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani  katika uteuzi wa kuwapata wagombea wa ubunge  wa bunge la Afrika Mashariki (EALA)   Chadema, CUF  na NCCR Mageuzi kwa jinsi walivyowasilisha  uwakilishi haba na finyu lakini pia kujitokeza kwa wagombea wachache hali inayoonyesha uminyaji wa demokrasia ndani ya vyama vyao.

Chadema na washirika wao mara kadhaa hujigamba vichochoroni na kujionyesha kuwa wao ni  watetezi  wa demokrasia lakini unapofikia wakati wa utekelezaji wa jambo hilo  kwa vitendo, ndani ya chama hicho humea ukandamizaji wa haki na kujitokeza  upendeleo, ukanda, kubebana  aidha kwa asili, ujamaa na urafiki au kulipana fadhila.

Katu huu si mwenendo mwema ulioonyeshwa na vyama vya upinzani. Vimejipaka matope ya fedheha kwa kushindwa  kuonyesha kama ni waumini wa kweli wa demokrasia badala yake havikujali wala kuheshimu dhana ya demokrasia na kujikuta  vimejianika na kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa  vyama hivyo ni vya watu maalum vya kibwanyenye na vya kiimla .

Kufanya uteuzi wa wanachama wanaogombea nafasi za kidemokrasia kwa kumtazama asili yake, anatoka  kanda ipi, kabila, imani yake au nasaba licha ya  kwenda kinyume na misingi ya Taifa letu lakini pia ni kinyume na matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM kwa kauli moja tunawaamsha na kuwatumia ujumbe watanzania wenzetu hususan Vijana mahali popote walipo wavikatae na kuvikwepa vyama vya aina hiyo, wasikubali kugawanywa kwa asili zao, imani au rangi na nasaba.

Taifa letu ni alama pana ya kuenzi na kudumisha demokrasia si tu barani Afrika lakini vile vile duniani kote, hivyo kwa umoja wetu, kwa nguvu zetu, akili na maarifa tulionayo, abadan tusijaribu kuichezea amani yetu, umoja na mshikamano wetu  uliojengwa na waasisi wa Taifa letu na kukubali  kuvishabikia vyama na viongozi wasaka madaraka kwa hila ambao ni  wafujaji na wakandamizaji wa misingi ya demokrasia ndani ya vyama kama ilivyojionyesha  kwa vyama vya upinzani vya Tanzania katika uteuzi wa wabunge EAC.

Mchakato wa Uchaguzi ndani ya UVCCM.

Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2017, unafanyika wakati ambapo CCM inatimiza miaka 40 tokea kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari, 1977 na ni wakati ambapo nchi yetu inatimiza miaka 25 ya Mfumo wa Vyama Vingi ulioridhiwa na Mkutano Mkuu wa CCM kutokana na busara za Viongozi wake.

Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Chama na Jumuiya zake inaonesha mchakato wa Uchaguzi wa Jumuiya za CCM kuwa unaanza kabla ya ule wa CCM. Utaratibu huu unalenga kuwawezesha wanachama wa Jumuiya za CCM ambao watakuwa ni wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika CCM, au wale waliochaguliwa kuwakilisha Jumuiya zao katika Vikao vya CCM ili waweze kuhudhuria mikutano ya Chama inayowahusu.

Umoja wa Vijana wa CCM umekamilisha maandalizi yote ya msingi ya awali kwa ajili ya Uchaguzi unaotarajia kuanza tarehe 1 April, 2017 ikiwemo kusambaza vifaa katika Mikoa na Wilaya zote nchini wa ajili ya kufanikisha uchaguzi kwa wakati.

Aidha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imekamilisha mapitio na uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika Jumuiya ambao watakuwa ndio wakurugenzi wa Uchaguzi katika maeneo yao.

Tunaendelea kuwakumbusha Watendaji wetu muda wote kusimamia haki, ukweli na usawa lazima vijana wa CCM muda wote tuishi katika maneno na maagizo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

Hatutamvumilia mtendaji yeyote atakayekiuka Kanuni, Taratibu na miongozo kwa makusudi ili kufurahisha kikundi au watu fulani. Uchaguzi huu 2017 UVCCM tunataka kuidhihirishia dunia na Vyama vya Upinzani kuwa CCM ni Chuo Cha Demokrasia ulimwenguni.

Mwisho niendelee kuwahamasisha vyema wote nchini yenye sifa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

KAIMU KATIBU MKUU
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wana Habari Makao Makuu UVCCM Upanga (PICHA NA FAHADI SIRAJI)
Share:

Jumatano, 29 Machi 2017

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Machi 2017 ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.


Kikao cha Kamati Kuu kimepokea taarifa ya Mchakato wa wanachama na makada wa CCM wanaoomba ridhaa na dhamana ya kuwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. 

Wajumbe wa Kamati Kuu wametafakari kwa kina wa wameridhishwa na uwazi wa mchakato mzima na namna ambavyo chama kimeonesha demokrasia pana, komavu na shirikishi. Katika mchakato huu jumla ya wanachama na makada 450 walijitokeza, wanawake wakiwa 93 na wanaume 357, wengi wakiwa na elimu ya kuanzia Chuo na Chuo Kikuu. 
Chama cha Mapinduzi katika kuzingatia Usawa wa wanawake na wanaume, imefanya uteuzi wa wana CCM 12 kwa mchanganuo wa Bara Me(4) na Ke(4) na Zanzibar Me(2) na Ke(2) ambao majina yao yatawasilishwa Bungeni kwa Uamuzi wa mwisho. Pia chama kimewapa Pongezi sana wana CCM wote ambao wameomba ridhaa 

*WALIOPATA UTEUZI KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM) ILI KUOMBA RIDHAA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI*

*TANZANIA BARA*
WANAWAKE 
1.Zainabu Rashid Mfaume KAWAWA 
2.Happiness Elias LUGIKO 
3.Fancy Haji NKUHI 
4.Happiness Ngoti MGALULA 

WANAUME 
1.Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE 
2.Adam Omari KIMBISA 
3.Anamringi Issay MACHA 
4.Charles Makongoro NYERERE 

*TANZANIA ZANZIBAR*
WANAWAKE
1.Maryam Ussi YAHYA 
2.Rabia Abdalla HAMID 

WANAUME 
1.Abdalla Hasnu MAKAME 
2.Mohamed Yussuf NUH
Share:

Jumatatu, 27 Machi 2017

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG), IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MARCH 27,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam March 27,2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anapiga makofi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hiyo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Alphayo Kidata pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo kutoka kwa CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
Share:

Ijumaa, 24 Machi 2017

Alhamisi, 23 Machi 2017

RAIS MHE. DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI NA KUZUIA MAKONTENA 20 YENYE MCHANGA WA MADINI ULIOKUWA USAFIRISHWE NJE YA NCHI MARCH 23,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusu makontena 20 yenye mchanga wa madini uliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari pamoja na vitu vilivyochakaa March 23,2017


Moja ya kontena likiwa lina magari matatu ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake wanakuwa wameficha magari ya kifahari.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo.PICHA NA IKULU
Share:

Jumatano, 22 Machi 2017

KATIBU IDARA YA OGANAIZESHENI CCM PERREIRA AME SILIMA AKABIDHIWA OFISI RASMI,LEO OFISI NDOGO CCM LUMUMBA DAR ES SALAAM.


Aliyekuwa Katibu wa Idara ya Organization Chama Cha Mapinduzi Dkt Mohammed Seif Khatib akizungumza wakati wa Makabidhiano ya Kiofisi na Katibu Mpya Idara ya Organization CCM ndg:Perreira Ame Silima,Leo Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
Katibu Idara ya Organization  CCM Ndg:Perreira Ame Silima akisain Hati ya Makabidhiano ya Vifaa mali, na Majukumu ya Chama Idara Ya Organaizeshen uku Maafsa wa chama wakishuhudia Zoez hilo,Leo Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
 Katibu Idara ya Organization  CCM Ndg:Perreira Ame Silima wa kwanza kushoto akikabidhiwa Hati ya Makabidhiano ya Vifaa mali, na Majukumu ya Chama Idara Ya Organaizeshen  na Dkt Mohammed Seif Khatibu aliyekuwa  Katibu Idara ya Organization  CCM uku Kaimu Mkuu wa Idara ya Organaizeshen na Siasa UVCCM TAIFA Ndg:Pili Agustino akishuhudia Makabidhiano hayo,Leo Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
  Katibu Idara ya Organization  CCM Ndg:Perreira Ame Silima wa kwanza kushoto akikabidhiwa Kanuni za Chumuiya za Chama  na Dkt Mohammed Seif Khatibu aliyekuwa  Katibu Idara ya Organization  CCM uku Kaimu Mkuu wa Idara ya Organaizeshen na Siasa UVCCM TAIFA Ndg:Pili Agustino akishuhudia Makabidhiano hayo,Leo Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
 Katibu Idara ya Organization  CCM Ndg:Perreira Ame Silima wa kwanza kushoto Akikabidhiwa Funguo  na Dkt Mohammed Seif Khatibu aliyekuwa  Katibu Idara ya Organization  CCM uku Kaimu Mkuu wa Idara ya Organaizeshen na Siasa UVCCM TAIFA Ndg:Pili Agustino akishuhudia Makabidhiano hayo,Leo Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
picha ya pamoja  Katibu Idara ya Organization  CCM Ndg:Perreira Ame Silima wa kwanza kushoto na DktMohammed Seif Khatibu aliyekuwa  Katibu Idara ya Organization  CCM(PICHA ZOTE NA FAHADY SIRAJI )
Share:

Jumatatu, 20 Machi 2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA ZA JUU (INTERCHANGE) KWENYE MAKUTANO YA UBUNGO MARCH 20,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwa wamepanda basi la mwendokasi huku wakibadilishana mawazo wakielekea Ubungo kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kabla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilia Prof. Makame Mbarawa kwa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim walipokwenda kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi alipokwenda kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakifungua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakipata maelezo jinsi barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo zitakavyokuwa baada ya kujengwa March 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye Makutano ya Ubungo March 20,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye Makutano ya Ubungo March 20,2017

 PICHA NA IKULU
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu