Unordered List


CCM Z’BAR YATAKA TAASISI ZAKE KUBUNI MIRADI ENDELEVU YA KIMAENDELE.

mab1
Jengo jipya la CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Kichama lililopo katika kijiji cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini  “B”  Unguja.
mab2
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla “Mabodi” akizungumza na uongozi wa  Mkoa huo mara baada ya kukagua jengo hilo wakati alipokuwa katika ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Mkoa huo.
mab3
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Bw. Haji Juma Haji akitoa ufafanuzi  juu ya mambo mbali mbali yanayohusu jengo hilo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla “Mabodi”  alipokuwa katika ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Mkoa huo.
mab4
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Bw. Haji Juma Haji akitoa ufafanuzi  juu ya mambo mbali mbali yanayohusu jengo hilo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla “Mabodi”  alipokuwa katika ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Mkoa huo.
…………………………………………………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadalla “Mabodi”  amewaagiza  Watendaji na Viongozi wa Chama na Jumuiya zake kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya kudumu ya kimaendeleo.
Agizo hilo amelitoa katika ziara yake huko Mkoa wa Kaskazini Unguja alipotembelea jengo jipya la kisasa la  ofisi ya Mkoa huo, huko Mahonda Unguja, alisema jengo hilo limekamilika kwa muda mwafaka ambao Chama hicho kipo katika mkakati maalum wa kuwa na vitega uchumi imara vitavyosaidia chama kujitegemea  katika masuala ya kiuchumi.
Dkt. Mabodi alieleza kwamba Chama hicho kwa Zanzibar lazima kila ngazi ya kiutendaji kuanzia katika Mashina hadi Taifa ni lazima wawe na miradi ya maendeleo kupitia rasilimali ardhi na baadhi ya majengo waliyokuwa nayo ili waweze kujipatia kipato kitakachosaidia kutatua changamoto za ukata wa fedha hasa katika masuala ya kiutendaji na kijamii.
Aliwambia wanachama CCM Zanzibar kwamba nia ya muundo na marekebisho ya Katiba ya Chama ni kuhakikisha utamaduni wa chama kutegemea ruzuku za serikali sambamba na ngazi zote za chama na jumuiya kuona zinaanza mapema kujiandaa kisaikolojia kwa kuanzisha miradi na vitega uchumi.
“ Kwanza nakupongezeni kwa juhudi zenu za kujenga jengo la kisasa la ofisi linaloendana na hadhi ya CCM, lakini kubwa ni kwamba ndani ya jengo hili mmeweka vitega uchumi vya kuzalisha mapato yatakayosaidia katika shughuli za uendeshaji.
Rai yangu kwenu na Mikoa mingine ya Kichama pamoja na Jumuiya zake, tuanze rasmi kuenzi busara za Waasisi wetu ambao ni Marehemu Abeid Amaan Karume na wenzake ili serikali na chama tawala vijitawale kiuchumi na kimaendeleo.”, alisema Dkt. Mabodi.
Akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Haji Juma Haji alisema jengo hilo limejengwa kwa juhudi za ungozi wa Mkoa huo kwa kushirikiana na wanachama wengine waliokubali mwekezaji ajenge jengo hilo ili wapate fursa mbali mbali za kiuchumi.
Bw. Haji pia aliweka wazi kwamba licha ya kuwepo na vikwazo vya majukungu na kauli zisizofaa kutoka kwa baadhi ya wapinga maendeleo, lakini wameweza kulikamilisha na kwa sasa kilichobaki ni kuwekwa vifaa vya samani ili liweze kuzinduliwa rasmi.
Akitoa ufafanuzi juu ya jengo hilo, Katibu wa CCM Mkoa huo,  Bw. Mulla Othman Zubeir  amesema jengo hilo limeanza kujengwa toka  mwaka 1986 na baadae liaachwa lakini uongozi wa mkoa huo wa sasa uliamua kuliendeleza  kwa msaada wa Mwekezaji  ambaye ni Bw. Braiyan Somson  kupitia mradi wake wa Pen Royal ameweza kujenga jengo hilo bila masharti yoyote.
Katibu Bw. Mulla alieleza kwamba Mwekezaji huyo amekuwa ni miongoni mwa watu muhimu waliosaidia kufanikisha ofisi hiyo ya kisasa kwani ameonyesha mapenzi na nia ya kweli ya kukiunga mkono chama cha Mapinduzi.
Ofisi hiyo imejengwa kwa gharama zinazokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 300 pia ina  vitengo vyote Chama na Jumuiya zote kwa ngazi mbali mbali za Mkoa huo pamoja na vyumba vya ukodisha maduka ili mkoa huo upate fedha za kuongeza kipato katika shughuli za kiutendaji.

Chapisha Maoni

0 Maoni