Na Mwandishi Wetu,Katavi
Chama
cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mpanda Mkoani hapa kimesifu
marekebisho ya katiba ya ccm yaliopitishwa na mkutano mkuu na
kusema
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli apewe muda wa kutekeleza
majukumu na malengo yake kisiasa na kiserikali .
Hayo
yamelezwa jana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Beda Katani
kabla ya kumkaribisha kaimu katibu mkuu wa Uvccm shaka hamdu Shaka
alipozumgumza katika kikao cha ndani na wananchama wa ccm katika ofisi
za chama kijiji cha Ifukuto kata ya Pandambili Mkoani hapa
Beda
alisema kila zama huwa na nabii na kitabu chake hivyo kwakuwa wananchi
katika jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi sasa Rais wao ni Dk
Magufuli , apewe muda na wasaa mpana kusimamia malengo na mipango ya
serikali yake.
Alisema
unapoyapitia na kuyasoma mabadilko ya katiba ya ccm yaliopitishwa na
wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa yamebeba dhana ya kuleta mageuzi ya
kisiasa pia jinsi serikali inavyowajibika kwa wananchi ni mambo
yakuungwa mkono badala ya kubezwa.
"Tumepata
Mwenyekiti imara na Rais mchapakazi , nafikiri tumpe nafasi ajipambanue
ili atimize malengo yake,anafanya mambo ambayo sasa hayaonekani kwa
macho . Iko siku wananchi watajua"Akieleza Mwenyekiti huyo .
Kwa
upande wake Katibu mpya wa ccm wilaya ya Tanganyika Selemani Majilanga
alisema kuhamishwa kwake katika wilaya hiyo atahakikisha anawaunganisha
na kuwaweka pamoja wanachama wote kwakuwa hapendi mgawanyiko.
Majilanga
aliwahakikishia wanaccm wilaya ya Tanganyika kwamba kazi ya siasa bila
kuwepo ushirikiano, upendo, usiri na wanachama wenyewe kujitolea hawezi
kuwaletea tija au manufaa wanachana na wananchi.
"Nitafanya
kila nitakaloweza kuhakikisha tunasimamia pamoja malengo ya chama, bila
ya kuwepo uongozi na uhai wa chama hiki hali ya usalama nitulivu
inaweza kuvurugika, utulivu na amani ni matokeo ya sera bora za
serikali ya ccm "Alisema .
Akizungumza
katika mkutano huo Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
aliwataka viongozi kuongeza nguvu ya ushirikiano, kufanyakazi pamoja pia
kushughukia kero na shida za wananchi kwa sauti moja.
Shaka
alisema ikiwa wananchi kwa hiari yao wameiweka kidemokrasia madarakani
serikali ya ccm na kuiamini, kutokana na uzoefu walionao viongozi
wake,wanachama na viongozi wa CCM wajione wana haki ya kuenzi heshima
hiyo.
"Pigeni
mzigo viongozi kwa kuwashirikisha wanachana wenu, CCM ikiwa ya kwanza
kukemea ubadhirifu, wizi, udokozi na ufisadi,wananchi watajenga imani na
kuona chama chao kinawatetea na kuwapigania "Alisema Shaka.
Alisema
kazi ya kusimamia serikali ili itimize majukumu yake ya kisera ni ya
ccm hivyo ikiwa viongozi wa chama wanaona mambo yanakwenda ndivyo sivyo
huku nao wakinyamaza kama hawapo au hawaoni yanayofanyika wananchi
hawatajua thamani, ubora na umuhimu wao.
"Hapa
kwenu pia zipo serikali ,zipo za vijiji na viongozi.,yupo Afisa
mtendaji kata, katibu Tarafa , Dc na Ded, hao wote ni vyombo vya
dola,kwanini mambo yaharibike mbele yao, chama sasa kisimamie ili
kuhakiksha mambo yanafuata mkondo wake "Akieleza Shaka
(picha na fahadi siraji)
0 Maoni