Unordered List


JOKATE URBAN MWEGELO KUIWAKILISHA UVCCM KUAGA MIILI YA WANAFUNZI WALIOFARIKI ARUSHA KWA AJALI YA GARI


Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndg:Jokate Mwegelo atawakilisha Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Katika Kuaga Miili ya Wanafunzi waliofariki kwa ajali ya gari tukio litakalo fanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kesho tar8/05/2017

  Akiwasili Uwanja wa ndege wa KIA Ndg:Jokate Mwegelo, Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana wa CCM amepokelewa na ndg:Saitoti Steven Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha pamoja na Viongozi mbalimbali wa UVCCM Mkoa wa Arusha
   
  Hapo kesho Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi uvccmNdg:Jokate Mwegelo
akiiwakilisha UVCCM  katika kuaga miili ya Wanafunzi walio fariki katika ajali ya gari ataungana na Makamo wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Samia Suluhu Hasan ambaye pia amewasili Mkoan humo jion ya leo kwa ajili ya kuongoza Mamia ya waombolezaji Mkoa wa Arusha na Mikoa Jiran pamoja na Ndugu,jamaa na Marafiki katika familia mbali mbali za Marehemu hao

bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe

Chapisha Maoni

0 Maoni