Sent from Samsung Mobile
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
alipotembelea miradi wa ujenzi wa madarasa mawili, vyoo matundu 16 na
jengo moja la nyumba ya walimu lenye vyumba sita katika kijiji Ipwaga
Kata Ilela wilayani Mlele Mkoani hapa .
Na Mwandishi Wetu, Katavi
Halmashauri
za Wilaya zimetakiwa kujenga umakini, uaminifu , usimamizi na matumizi
bora wa rasilimali fedha ikiwemo zile zinazoletwa na Serikali Kuu au
misaada inayotolewa na Mashirika au Taasisi za Kimataifa.
Hayo
yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
alipotembelea miradi wa ujenzi wa madarasa mawili, vyoo matundu 16 na
jengo moja la nyumba ya walimu lenye vyumba sita katika kijiji Ipwaga
Kata Ilela wilayani Mlele Mkoani hapa .
Shaka
alikitaja kiasi kilichotajwa cha shilingi milioni 247 kutumika katika
ujenzi huo ni kikubwa ukilinganisha na thamani ya majengo yalivyo hivyo
akawataka madiwani na halmshauri ya Mlele kuwa makini na kuepuka
matumizi mabaya ya rasilimali fedha.
Alisema
katika hali ya kawaida kiasi kilichotumika kujenga majengo hayo ni
kikubwa kuliko ubora na ukubwa wa majengo yenyewe yanavyoonekana na
inamshawishi mtu yoyote aamini huenda katika ujenzi huo kulipita ufisadi.
"Hatuwezi
kuwakabili wananchi na kuwaambia majengo haya ujenzi wake umegharimu
milioni 247, watatuona hatuko makini , nadhani hapa kuna harufu ya
ufisadi na ubadhirifu wa fedha "Alisema
Alimueleza
Diwani wa Kata ya Ilela William Miula kwamba aina ya utendaji huo
unaweza kuigombanisha Serikali na wananchi hatimaye viongozi wote
wakaonekana ni wezi na hawajali katika kusimakia maslahi ya umma.
"Nitakutana
na Waziri dhamana wa Tamisemi kumjulisha jambo hili, tukiyafumbia macho
uzembe huu hatutaweza kukomesha wizi na udokozi wa mali za umma, hivi
kwanini tunashindwa kuwa wakweli na kukosa uaminifu "Alihoji Shaka huku
akionekana kukerwa na taarifa hiyo.
Awali Shaka alishiriki ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi
katika Kijiji cha Mlogoplo Kata Ilela
na kuchangia mifuko 20 ya saruji huku akiwataka wananchi kujenga hali ya kujitolea na kushiriki kazi za ujenzi wa Taifa.
Alisema
jukumu la kujitolea kwa maslahi ya Taifa litabaki kuwa mikononi mwa
wananchi wenyewe bila ya kusubiri misaada aidha ya wahisani , wafadhili
au mashirika yasio ya kiserikali .
Pia
aliwahimiza wananchi katika kijiji cha Mlogolo kuelewa kuwa juhudi
zozote watakazochukua ni kwa manufaa ya watoto na vizazi vyao hivyo
akasema kujitolea kunaonfeza kasi ya maendeleo.
"Nchi
yetu itajengwa na sisi wenyewe, mwenye mawazo kama yupo mtu atakuja
kutuletea maendeleo anajidanganya mwenyewe, tufanye kazi kwa bidii ,
tumuunge mkono Rais wetu Dk John Magufuli katika kauli mbiu ya hapa kazi
tu 'Alieleza shaka
0 Maoni