Jumatano, 3 Mei 2017

UVCCM:JIOGRAFIA YA KATAVI NI KIMBEMBE

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizumguza na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa na kamati za utekelezaji za jumuiya  Mkoa wa Katavi mbele ya Mwenyekiti  wa CCM mkoa huo Mselem Abdallah Mselem katika ofisi za chama.


Na Mwandishi  Wetu, Katavi


Umoja wa Vijana wa CCM umekipongeza Chama Cha Mapinduzi Mkoa  wa Katavi kwa juhudi, mikakati na mipango yake ya muda mfupi na mrefu ya kukijenga na kukipeleka mbele chama hicho ili kuwa karibu na wananachi ikiwemo kutambua matatizo yanayowakabili .

Pia umoja huo umesisitiza kuwa pamoja na jiografia ya Mkoa huo kuwa ngumu  bado viongozi  na watendaji wa chama na jumuiya zake wameendelea kufanya kazi za kisiasa bila kuvunjika moyo.

Hayo yameelezwa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati alipozumguza na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa na kamati za utekelezaji za jumuiya  Mkoa wa Katavi mbele ya Mwenyekiti  wa CCM mkoa huo Mselem Abdallah Mselem katika ofisi za chama hicho mkoani hapa. 

Shaka aliwataka viongozi na watendaji wa chama na jumuiya zake kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake wa kisiasa, kiutumishi na kiajira kwasababu dhamana ya kila kiongozi ni kuutenda, kuwajibika na kukisaidia chama.

Alisema kazi ya siasa ni ya kujitole kwa moyo, upendo, ukereketwa na uzalendo hivyo kiongozi au mwanachama anayeingia katika siasa kwa tamaa ya kulipwa posho, hatoshi na hafai kubaki na kujiita mwanasiasa .

"Jiografia ya mkoa Katavi ni ngumu huku mazingira yake kimawasiliano pia ikitatiza, hatuna budi ila kila mmoja wetu ajitume na kutimiza wajibu wake, chama na nchi yetu itajengwa na wale wote wenye kujituma "Alieleza shaka 

Aidha akizungumzia uchaguzi unaoendelea katika ngazi mbalimbali za chama na jumuiya, alisema wakati huu ni muhimu ili kupata viongozi bora, makini na wenye ari ya kukitumikia na kuietea  ccm mahali popote. 

Alisema wanachama wajitokeze kwa wingi ili kuchukua fomu za kuwania uongozi katika ngazi zote kwa sababu kila mwanachama wa CCM  ana wajibu na haki ya kikatiba kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote. 

Pia shaka aliwataka na kuwahimiza watendaji wa chama na jumuiya zake kuhakiksha wanasimamia vyema uchaguzi huo kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na chama bila kukiukwa. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa Katavi Mselemu, alisema ingwaje kuna masafa na umbali mirefu  toka eneo moja kulifikia jingine, viongozi na wanachama wa CCM na jumuiya zake mkoani huko wameendelea kukiunga mkono chama hicho. 

"Mkoa wetu ulikua  mmoja Rukwa, umekatwa na kuzaliwa mpya wa Katavi, tumekuja kuanzisha upya harakati za ujenzi na maendeleo ya chama chetu, tumejitahidi  kufanya kila linalobidi na sasa tumepata ofisi, malengo yetu ni kujenga ofisi ya ghorofa "Alieleza Mselem. 

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi Kajoro Vyohoroka alisema chama chochote cha siasa na viongozi wake lazima wajipe jukumu la kujitegemea badala ya kujenga dhana au taaswira ya utegegemezi .

Vyohoroka alisema midhali serikali kwa mujibu wa sheria imewapatia wananchi wa katavi mkoa  mpya, wajibu na dhima sasa ya kuujenga na kuuendeleza kijamii na kiuchumi itabaki mikononi mwa wanachama na wananchi wa mkoa huo. 

Shaka  amechangia millioni mbili kuunga mkono ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM  mkoa wa Katavi kisha ameondoma na msafara w kuekewa wikaya ya Tanganyika baadae ataendelea ziara hiyo  katika wilaya nyingine za mkoa huo akizindua miradi ya maendeleo na kukagua uhai wa chama na jumuiya zake.


End 
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu