Unordered List


VIJANA NA FURSA :MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUANZA MAFUNZO KATIKA SEKTA ZA TEHAMA, UMEME, UCHOMELEAJI, UJENZI, USEREMALA, UFUNDI BOMBA, TERAZO, UFUNDI MAGARI, UCHONGAJI VIPURI NA USHONAJI NGUO.

''Tunaipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa kwa uweledi na uadilifu hasa katika kutimiza wajibu wake katika kuwezesha vijana wa kitanzania kama nguvu kazi ya taifa kupata fursa mbalimbali kupitia Wizara inayoshughulikia masuala ya vijana na Ajira.Kupitia Idara ya Ajira kutakuwa na mafunzo maalumu ya ufundi.Tunazidi kuwaomba waendelee kufikia vijana wengi zaidi ili sote tuweze kuiendeleza nchi yetu  kupitia vipaji vyetu.Tutaendelea kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi inasimamiwa na serikali yetu kwa kuwa daraja kwa vijana wenzetu kwa viongozi wa juu ili kuleta kwa viongozi wa juu ili kuleta maendeleo.Hapa kazi  Tu!!''Jokate Mwegelo Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa


 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


 


OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

TAARIFA KWA UMMA
KUITWA KUANZA  MAFUNZO YA STADI ZA KAZI KATIKA SEKTA ZA  TEHAMA, UMEME, UCHOMELEAJI, UJENZI, USEREMALA, UFUNDI BOMBA, TERAZO, UFUNDI MAGARI, UCHONGAJI VIPURI NA USHONAJI NGUO
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inapenda kutaarifu umma wa watanzania kuwa vijana 3,440 walioainishwa hapa chini wamechaguliwa kujiunga na mafunzo tajwa hapo juu. Mafunzo haya yamelenga kuwezesha nguvu kazi ya taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira na kuwezesha vijana kushiriki katika kukuza Uchumi wa Viwanda. Mafunzo haya yatatolewa katika Vituo vya Mafunzo vya Don Bosco vifuatavyo : Don Bosco VTC Oysterbay Dar es Salaam,  Don Bosco Upanga Dar es Salaam, Don Bosco Temeke Dar es Salaam, Don Bosco VTC Dodoma, Don Bosco VTC Iringa, Don Bosco Mafinga, Don Bosco Didia - Shinyanga na Don Bosco Moshi. Vijana wote waliochaguliwa watatakiwa kufika kuanzia mafunzo  kuanzia tarehe 29/05/2017 hadi 03/06/2017. Serikali itagharamia ada ya mafunzo pamoja na nauli wakati wa mafunzo ya shilingi 100,000 (Laki Moja tu) kwa kijana kwa mwezi. Aidha, gharama nyingine za kujikimu zikiwemo malazi na chakula zitagharamiwa na mwombaji au Mzazi/Mlezi. Majina ya vijana na vituo walivyopangiwa ni kama ifuatavyo.
MAJINA YA  VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO KATIKA FANI YA  UFUNDI UMEME - DON BOSCO OYSTERBAY
NA
JINA
JINSI
FANI
SEHEMU ANAKOTOKA
1
ABDALAH M . SOBO
M
ELECTRICAL
ILALA
2
ABDALAH S DUDU
M
ELECTRICAL
TEMEKE
3
ABDALAH S. ZUBERI
M
ELECTRICAL
TEMEKE
4
ABDALLAH AMAN
M
ELECTRICAL
ILALA
5
ABUBAKARI M. MAHULU
M
ELECTRICAL
TEMEKE
6
AKBAR H. KHAMISI
M
ELECTRICAL
UBUNGO
7
ALOYCE S. MBOYA
M
ELECTRICAL
KINONDONI
8
AMIRI H. IBRAHIM
F
ELECTRICAL
TEMEKE
9
ANAMARY MLYUKA
M
ELECTRICAL
ILALA

Chapisha Maoni

0 Maoni