Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na
Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
Alimueleza balozi huyo kuwa Serikali imebaini na itakomesha ujanja
unaofanywa na wafanyabiashara haramu wa kutakatisha fedha kwa kununua
makundi makubwa ya mifugo na kuyachunga kwenye maeneo ya hifadhi nchini
na baadae kuyauza kwa faida kwenye minada.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akifurahia jambo
na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi
Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke majarida mbalimbali enye taarifa
za vivutio vya Tanzania ofisini kwake mjini Dodoma. (Picha na Hamza
Temba – WMU)
0 Maoni