Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akikagua chumba cha upasuaji kilichopo katika
moja ya kituo cha Afya wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo ya kutolea huduma katika Hospitali ya Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akikagua mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya
kielektroniki katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe pamoja na
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Frank Bahati katika ukaguzi wa miradi ya
Afya.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Afya wilayani Ukerewe.
…………………………………………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo amewajia juu Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya(DMO),
Afisa Manunuzi, na mwakilishi wa Mweka hazina wa halmashauri ya wilaya
ya ukerewe baada ya kushindwa kutoa ufafanuzi sahihi juu ya ununuzi wa
dawa chini ya mfuko wa Afya wa pamoja (Busket Fund).
Akiwa katika ziara yake ya
kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, Jafo amefika
kwenye hospitali ya wilaya ya ukerewe na kuwaomba wananchi waliokuwepo
hospitalini hapo kueleza changamoto wanazozipata wanapofika hospitalini
hapo.
Kufuatia changamoto walizoeleza
wananchi, Jafo alionyesha kukerwa kutokana na maafisa hao kushindwa
kujibu hoja ya wananchi waliokuwa wakilalamika kwamba wanapofika kwenye
hospitali hiyo mara nyingi wataalam wamekuwa na kauli mbaya sambasamba
na kukosa dawa.
Jafo aliwageukia wataalam hao
kwa kuwauliza ni kiasi gani cha fedha za basket fund wamepokea kwa mwaka
Fedha 2016/2017 na kiasi gani kilitumika kununua dawa na vifaa tiba.
Kutokana na Jafo kuhoji fedha hizo, wataalam hao wote walishindwa kufahamu, jambo lililomkera Naibu Waziri Jafo.
Alisema ameshangazwa na kitendo
cha wataalam wahusika kushindwa kutambua mambo ya msingi ambayo
wanapaswa kuyasimamia ili kutatua kero ya afya kwa wananchi.
Jafo aliwajulisha wananchi kuwa
halmashauri yao imepokea jumla ya sh.milioni 727.4 ambapo 33% ilipaswa
kununulia dawa na vifaa tiba.
Naibu Waziri Jafo amewataka
watumishi wote kusimamia mipango ya serikali ili kutatua kero za
wananchi ili kuleta maendeleo katika jamii.
0 Maoni