Jumapili, 16 Julai 2017

SHAKA APOKELEWA KWA SHANGWE MKOANI KIGOMA

 Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (kushoto)akisalimiana na Katibu wa CCM Wilaya ya UVINZA ndg Evarist Mkuluge alipopokelewa Katika kata ya Nguluka Wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.
 Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (kushoto)akivalishwa Skafu
 Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (katikati) akikaribishwa rasmi na gwaride la vijana wa Green Guard Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
 Shamrashamra za Vijana wa Boda boda katika mapokezi ya Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
 Shamra Shamra za wanachama wa Chama cha mapinduzi katika mapokezi ya Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
 Katibu wa Chama cha mapinduzi Wilayani Uvinza akiwasilisha taarifa Utekelezaji pamoja na maendeleo ya uchaguzi wa Chama Wilayani Uvinza katika Ukumbi wa CCM NGULUKA
 Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM)mkoa wa kigoma ndg:Peter Joseph Msanjira akizungumza katika mkutano wa Ndani  uliofanyika katika ukumbi wa CCM NGULUKA.
Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM Wilaya ya Uvinza Mkoan Kigoma katika mkutano wa Ndani  uliofanyika katika ukumbi wa CCM NGULUKA.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)


.........

Na mwandiahi Wetu, Uvinza

Kaimu katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka leo amewasili na kupokewa kwa nderemo, vifijo,  hoihoi na shamrashamra katika kijiji cha Uvinza wilaya ya Uvinza Mkoani kigoma. 

Mamia ya wananchi wamejitokeza kwa wingi kumlaki  kiongozi huyo na kusimamisha shughuli kadhaa kwa muda kwenye mitaa wakati alipoingia majira ya saa 8.15 mchama mara baada ya kuvikwa skafu na chipukizi wa ccm wilayani Uvinza alikwenda moja kwa moja katika ofisi ya ccm wilayani hapa.  

Msafara wake ulioongozwa na bodaboda na ngoma za kienyeji ukipita mitaani kuelekea katika ofisi za ccm wilaya ya Uvinza ukiongozwa na viongozi wa Jumuiya na Chama. 

Mwwnyeliti wa CCM wilaya ya Uvinza Mohamed Kabamve , Katibu wa CCM  wilaya ya Uvinza Enerst Mruge , Katibu wa UVCCM mkoa Kigoma Stephen Koye Na katibu wa UVCCM wilaya ya Uvinza Adam Mikidad walikuwepo katika mapokezi hayo huku vijana wa Green Guard wa CCM na chipukizi wakiupamba msafara huo huku wakiwa wamevalia sare zao za kijani na weusi .

Shaka atakuwa Mkoani kigoma kwa ziara ya siku tano akitembelea wilaya za Uvinza, kigoma Mjini na Kakonko akizumgumza na wanachama wa ccm na jumuiya zake katika mikutano ya ndani akiimarisha uhai wa chama, kutembelea miradi ya maendeleo na kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm ya Mwaka 2015/2020 .

Kikundu cha ngoma ya kienyeji kiitwacho Tatu Bila ndicho kilichokuwa kikitumbuiza wakati shaka alipowasili wilaya hapa na kuwafanya watu kutibwirika bila kujali jua kali lililokuwa likiwaka.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu