Unordered List


UVCCM KATA YA CHAMAZI YACHANGIA CHAKULA KIKUNDI CHA VIJANA CHA PROFIT KILICHOPO MBANDE RUFU

Na Mwandishi wetu, Chamazi

Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi ukiongozwa na Mwenyekiti Nasri Bakari na Katibu Juma Bega Zonzo sambamba na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam UVCCM Ndg. George Madaraka leo wametembelea na kuchangia kikundi cha vijana wanaojihusisha na sanaa ya uigizaji, ngoma,uimbaji na waelimishaji wa stadi za maisha kinachoitwa PROFIT Kilichopo Chamazi Rufu jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo umoja huo ulichangia chakula kwa vijana 27 wa kikundi hicho waliopo katika zoezi la uchukuaji matukio kwa ajili ya tamthilia wanayoindaa jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa kwao.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Ndg. Nasri Bakari aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuweza kujiingizia kipato  sambamba na kuendana na usemi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa HAPA KAZI TU.

"Nawapongeza vijana kwa kuamua kuanzisha kikundi hiki, kwani kitawasaidia kuweza kupata kipato na hatimaye kupambana na adui mkubwa wa nchi yetu ambaye ni umaskini na hatimaye kuendana na kauli ya HAPA KAZI TU" alisema Nasri na kuendelea,

"Rais wetu anapambana sana kuhakikisha umaskini unaondoka hapa nchi na nyinyi mmeonesha kwa vitendo kumuunga mkono Rais wetu katika jambo hili mbarikiwe sana ".

Pia Katibu wa UVCCM wa Kata hiyo Ndg. Juma Bega Zonzo aliwapongeza vijana hao kwa kuanzisha kikundi hicho kwani kitawasaidia kupata kipato na kuwafanya wawe watulivu na wasikivu na hatimaye kufanya mambo yanayoipendeza jamii

Aidha Ndg. Juma Zonzo aliwasisitiza vijana hao kuwa mabalozi wazuri kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla na kuwaahidi kuwa UVCCM Chamazi itakuwa nao bega kwa bega na kuhakikisha ndoto zao zinatimia" alisema Ndg. Begga.

Akizungumza baada ya kupokea mchango huo Mwenyekiti wa kikundi hiko Ndg. Emmanuel Laiton ameushukuru uongozi sambamba na wanachama wa UVCCM Kata ya Chamazi kwa kuwatembelea na kujionea changamoto zao na hatimaye kuzitatua kwa wakati.

Chapisha Maoni

0 Maoni