Unordered List


UVCCM YAPONGEZA MIKATABA YA MAFUTA KUPITIWA ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya CCM (UVCCM) imepongeza msimamo kabambe uliotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu mkakati wa kujenga umakini katika uingiaji na kusaiji mikataba ya uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kabla ya uzalishaji wake kuanza visiwani humu.
UVCCM imesema hiyo ndiyo njia pekee muhimu na bora kuliko zote inatakayoleta manufaa na kutetea maslahi ya jamii ikiwa mikataba yote toka sasa itasimamiwa kwa weledi, umakini na uzalendo.

Tamko hilo limetolewa  na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg.Shaka Hamdu Shaka mara baada ya hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed  Shein aliyoitoa katika Baraza la eid el Fitry katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakikishi mtaa wa Maisa Suleiman  mjini Unguja.
Shaka alisema nchi za Afrika zimerudi nyuma sana kiuchumi na watu wake kubaki katika dimbwi la umasikini wa kutisha kutokana na baadhi ya viongozi wa serilali kutokuwa makini katika kusaini mikataba ya matumizi bora kwa  rasilimali za Taifa.

Alisema mpango mkakati uliotangazwa na Rais Dkt Shein kwa kuahidi kiwa serikali yake haitafanya mchezo katika upitiaji wa mikataba ,kusaini na kuanza kwa uchimbaji wa nishati hiyo na kutonufaisha kampuni pekee badala ya nchi, suala hilo ni muhimu kuungwa mkono na kutekekezwa ipasavyo wakati wake ukitimu.

“Nchi za kiafrika mungu ameziruzuku rasilimali na maliasili, hizo ni nyenzo za kujijenga kiuchumi na kupiga hatua kimaendeleo, mnapozubaa katika utiaiji saini mikatata, mnajikwamisha nyinyi wenyewe, matokeo yake tija  hubaki mikononi mwa watu wachache bila kuwanufaisha wananchi katika kupambana na umasikini “Alisema Shaka.

Alisema ikiwa kutakuwepo na umakini, mazingatio na uzalendo, nchi ndogo kama Zanzibar ni rahisi kupiga hatua na kujijenga kiuchumi pia watu wake wakatononeka kimaisha, wakaiishi kwa wasaa na kupata huduma bora za kijamii.
“Hotuba ya Rais Dk Shein katika Baraza la Idd  ilikuwa ya kizalendo ilitazama mbele katika siku nyingi zijazo na manufaa yake, amewaasa na kuwataka watendaji dhamana kujali nchi kwanza, haya ndiyo mambo yanaoyohitajiwa na wananchi, utaifa mbele na ubinafsi usipate nafasi “Alisisitiza.

Shaka alisema kitaaswira na kiuhalisia Rais anapigania maslahi ya umma na kuwaonya wale wote wenye mchezo wa tamaa ya kutaka kujinufaisha,  serikali yake haitawatazama na kufanya watakavyo hivyo jambo hilo kimsingi limeleta mjadala chanya.
“Kuna baadhi ya kampuni ambazo zina sera za kinyonyaji na utepeli , msipokuwa makini nyinyi wenyewe kwa kujipanga na kupigania maslahi ya umma, rasilimali zenu zitachotwa kiholela na umasikini wa watu utabaki pale pale daima dawamu, Dk Shein hataki hayo yatokee “Alieleza Kaimu huyo Katibu Mkuu.

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema wananchi katika Mataifa ya Afrika bado wanasakamwa na maadui umasikini. ujinga na maradhi huku  kwa miaka mingi mabeberu na wakoloni wmechota rasilimali za Afrika ili kuyaendeleza mataifa yao ,  kila nchi na serikali sasa ni vyema ikaweka mbele maslahi ya umma ikiwemo matumizi bora ya rasilimali “Alisisisitiza.
Alisema ingawaje maslahi na tija itakayopatikana katika uchimbaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia hufanyika katika nchi  za kiafrika, bila ya kuwepo utayari, umakini na uzalendo hata pale yamapochimbwa mafuta au madini, panaweza ndipo penye kitovu cha umasikini badala ya watu wake kupata huduma bora za kijamii.

Shaka alimsifu Rais Dk Shein kwa kulitazama kiundani suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa darubini kali na kuona mbali, jambo pekee lililobaki, alisema ni ufuatiliaji wa karibu katika kusainiwa mikataba hiyo ili kuipa faida Zanzibar na watanzania badala ya uchimbaji na uzalisjaji huo kubaki kama shamba lisilo na mwenyewe.
“Tunaamini uchimbaji wa mafuta na gesi asilia utakapoanza huku kukiwa na mikataba isio na ujanjaujanja itatoa nafasi  pana za ajira kwa vijana, kuongeza mapato kiuchumi na kuimarisha huduma za jamii, ahadi ya smz katika usimaiaji wa mikatata, UVCCM tumeopookea kwa macha mawili ” Alisema Shaka.

Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa waliohudhuria katika baraza la Eid Fitri liliofanyika katika viwanja wa baraza la wawakilishi la zamani Mnazimmoja Zanzibar.

Chapisha Maoni

0 Maoni