Jumanne, 4 Julai 2017

UVCCM:SUMAYE HAJUI MAANA NA DHANA YA DEMOKRASIA


Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )umesema Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye hafahamu wala hajui  mantiki  na  dhana ya demokrasia ya vyama vingi ndiyo maana amekua  akitoa  madai ya kitoto na shutuma za kuwepo   ukandamizaji wa demokrasia  nchini .

Kadhalia Umoja huo umeeleza kuwa kwakuwa Sumaye hajui na wala haelewi  mipaka na mizania itokanayo na demokrasia, amejikuta akiishutumu bila ushahidi serikali ya Rais Dk John Magufuli akiongozwa na msongo wa chuki, hamaki na choyo. 

Kaimu  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM  Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo jana aliposimama kusalimiana na Vijana wa CCM Mvomero Morogoro wakati akielekea Dodoma kufuatia madai ya Sumaye akidai watawala hawataki katiba mpya na nchi ina mfano wa mgumu wa vyama vingi vya siasa. 

Shaka alisema mantiki au msingi wa kuruhusiwa vyama vingi nchini si kukwamisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii au kuwafanya wananchi kila siku wakusanyike viwanjani kusikiliza mikutano ya hadhara bila kutilia maanani uzalishaji mali viwandani, mashambani na maofisini. 

Alisema aina yoyote ya demokrasia ambayo  itakakosa  ukomo , adabu,  mipaka. mizania  na ustaarabu, huweza kujibadili na kupoteza uhalisia wake au heshima katika jamii ikiwemo kuwafanya watu wasijue  uyakini wa dhana yenyewe. 

" Vijana wenzangu hata ligi ya soka au mashindano ya kutafuta warembo yana msimu na vipindi vyake, timu haziwezi kushiriki michuamo mwaka mzima bila wachezaji na waamuzi kupumzika, domokrasia ya wapi ambayo haina vipindi vya kampeni, uchaguzi au watu kutakiwa kufanya kazi za maendeleo acheni kusikiliza poroja za wanasiasa waliochoka vijana chapeni kazi sasa ili kujiletea maendeleo endelevu" Aliwasa Shaka .

Alisema UVCCM imeshangazwa na matamshi ya Sumaye anayedai kuwa serikali ya awamu ya tano inakandamiza  misingi ya demokrasia kwasababu tu imevitaka vyama kuendesha shughuli za kisiasa kwenye mikutano ya ndani ili kuwapa nafasi wananchi kujituma na kuzalisha. 

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema hata kanuni na fomula za masomo ya hesabu, kemia na baiolojia hazilingani katika kupata majawabu halisia hivyo akataka ifahamike  demokrasia nayo ina vipindi vya kampeni , mikutano ya hadhara, uandikishaji, upiga kura,kuhesabu na kutangazwa matokeo .

"UVCCM tunamfahamu Sumaye toka akiwa Naibu Waziri wa Kilimo hadi Waziri Mkuu, hana rekodi nzuri ya kiutendaji ilioleta tija, mafanikio au ufanisi katika maeneo  aliyoyaongoza, yaonyesha ni mshabiki wa hadithi kuliko kufanya kazi "Alisistiza.

Aidha alimtaka mwanasiasa huyo kufuta ndoto na fikra siku moja itatokea CCM kudondoka madarakani kisha yeye au mshirika wake Edward Lowassa mmoja kati yao  awe urais au mgombea yeyote kupitia Chadema na Ukawa .

"Tanzania imechoka kuwa ombaomba wa kila msaada toka kwa wahisani na washirika wa maendeleo, Serikali ya CCM  imezinduma usingizini na kujitambua, haitaruhusu upuuzi usio na manufaa ili ionekane  demokrasoa maana yake ni mikutano ya hadhara bila uzalishajimali nakutakeni vijana popote mlipo nchini kila mmoja  afanye kazi tumuunge mkono kwa vitendo Rais wetu Dk John Pombe Magufuli anawapenda sana vijana na anatamani kuona mnafanikiwa katika ndoto zenu za kuinua kipato kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii "Alisisistiza Shaka.

Kaimu huyo Katibu Mkuu alieleza kuwa Waziri Mkuu huyo Mstaafu anatatapata na kutoa matamshi yenye ukakasi unaoambatana na  fitna kwa matarajio ya kuzifarakanisha jumuiya za kimataifa na Serikali za CCM ili zionekane haziheshimu demokrasia wakati si dai la kweli. 

"Sumaye na Chadema wakati wakitoa matamshi hayo ya kitoto na  kudai demokrasia haipo bila katiba mpya, nchi wahisani, taasisi za nje, mashirika ya kimataifa na washirika wa maendeleo, wanapongeza utendaji wa Rais na Serikali yake" Alieleza 
Hata hivyo  Shaka alimtaka Sumaye kuachana na siasa za kizamani kwasababu hata ushiriki wake akiwa Chadema haumjengei heshima na uaminifu kutokana na udhaifu wa kumbukumbu zake toka akiwa kiongozi wa juu wa Serikali kabla ya kuhamia upinzani na kusaka madaraka huku akiwa hakubaliki. 

Sumaye mwishoni mwa wiki alitoa matamshi yanaiponda serikali ya ccm wakati akizungumza katika mahafali ya vijana wanafunzi wafuasi wa chadema (CHASO) jijini Dar es Salaam  huku akiinanga Serikali ya Rais Dk Magufuli kwa madai ya kukwepa kuhusisha  mchakato wa katiba inayopendekezwa na madai ya kukandamiza demokrasia  ya vyama vingi kwa   kuzuia  mikutano ya hadhara na maandamano ya amani. 
End 
Source Zanzibar Leo
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu