Unordered List


Huyu ndio Rais Magufuli

DAIMA NITAKUWA NAWE

Nina kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Rais wangu mpendwa Dk. John Pombe Magufuli kwenye kila hatua anayopiga anapoiongoza nchi yetu ya Tanzania, Nina kila sababu ya kubaki na Rais Magufuli.

Rais Magufuli tangu uingine nimekuwa shuhuda wa namna gani unavyotimiza ahadi yako ya kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Elimu hii bure hugharimu pesa nyingi, kiasi cha Tsh. Bilioni 18.77 kila mwezi ambazo Serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikizitoa ili Mimi, Wewe na yule tuwe wanufaika wa kumuangamiza adui ujinga.

Nimekuwa shuhuda namna Serikali ya Rais Magufuli inavyotoa mikopo ya elimu ya juu. Kwa mwaka 2017/18 Serikali ilitoa mikopo ya Tsh. Bilioni 483 kutoka mikopo ya Tsh. Bilioni 341 kwa mwaka 2015 wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani. Ongezeko hili la fedha limeongeza pia idadi ya Wanafunzi wanufaika wa mikopo hiyo. Kwanini nisimuunge mkono Rais Magufuli?

Serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kuula "mfupa mgumu" kwa kuhakikisha shule zinakuwa na madawati, maktaba pamoja na maabara.

Rais Magufuli amefanikiwa kupunguza kiwango cha rushwa nchini na kuongeza kiwango cha nidhamu na uwajijikaji kwa Watumishi wa umma maeneo ya kazi.

Rais Magufuli tangu aingie madarakani sioni tena yale manyanyaso ya mgambo kwa Wamachinga na Mama Ntilie wanaofanya biashara halali, sehemu halali.

Serikali ya Rais imefanikiwa kufufua mashirika ya umma yaliyokuwa shimoni ama yaliyokuwa njia moja kuelekea shimoni. Rais Magufuli amefufua Shirika la ndege la ATCL kwa kununua ndege 4 mpya, amefufua shirika la simu TTCL kwa kununua hisa zote na sasa linamilikiwa na Serikali na ufufukaji wake unaonekana.

Rais Magufuli ameendelea kukiboresha kilimo hapa nchini kwa kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati, amefuta kodi kero na mzigo kwa Wakulima. Nina kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameendelea kudhibiti mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 5.4 kwa mwezi Juni kutoka asilimia 6.7 mwaka 2015.

Hali hiyo imesababisha uchumi wa nchi kukua hadi kufikia asilimia 7.2 ambao ni ukuaji wa juu  kabisa ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais Magufuli tangu aingie madarakani madawa yamekuwa yakipatikana hospitali tena kwa bei nafuu. Vipimo, vifaa tiba na operesheni nzito zimekuwa zikifanyika hapa hapa nchini.

Utawala wa Rais Magufuli umeendelea na ujenzi wa miundo mbinu kama vile Barabara, viwanja vya ndege, madaraja, vivuko na reli. Mathalani upande wa reli kuna ujenzi wa reli ya kisasa kwa ujenzi wa standard gauge kuanzia Dar mpaka Moro kwa awamu ya kwanza. Reli hii ikikamilika itakuwa na kasi ya ajabu ya spidi 160 kwa saa. Nani kama Magufuli?

Ndio maana nazidi kusisitiza, daima nitakuunga mkono, daima nitakuwa nawe, daima nitabaki nawe Rais wangu mpendwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli

Na Emmanuel J. Shilatu
0767488622

Chapisha Maoni

0 Maoni