Unordered List


TFDA Yasitisha utoaji wa vibali vya uingizaji wa bidhaa za nyama kutoka Afrika Kusini

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imezuia uingizaji wa soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya listeria.

Uamuzi wa TFDA unatokana na soseji hizo aina ya Polony kubainika kuwa na aina hiyo ya bakteria wanaosababisha ugonjwa wa listeriosis uliosababisha vifo vya watu 180 nchini Afrika Kusini.

Soseji hizo kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo kadhaa vya kimataifa zinatengenezwa na kiwanda cha tiger brands unit enterprises na cha RCL foods vyote vya Afrika Kusini.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi alikaririwa na mitandao ya kijamii akisema ameagiza kuondolewa sokoni soseji hizo, huku akiwashauri wananchi kuacha kula.

Motsoaledi alisema ingawa kiwanda cha RCL hakijatajwa kama chanzo cha ugonjwa huo, kitengo chake kinafanyiwa uchunguzi.

Ugonjwa wa listeriosis uliibuka Desemba mwaka jana na umeshasababisha vifo vya watu 180.

Chapisha Maoni

0 Maoni