Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema unamheshimu sana Mkurugenzi wa kituo
cha sheria na Haki za binadamu LHRC Dk Hellen Kijo Bisimba ila kwa
matamshi ya kushutumu serikali bila ushahidi na kutotazama mambo upande
wa pili wa shilingi huenda utu uzima unamuelemea.
Aidha
UVCCM imesema kama Mkurugenzi huyo amefurahishwa na matamshi ya Mbowe
ya kutaka amani ivunjike , umwagaji damu utokee kama Misri na Libya ni
wazi mwanamama huyo amepoteza uwezo wake wa kupambanua mambo kwa haki .
Matamshi
hayo yametamkwa na Kaimu katibu Mkuu wa UVCCM shaka Hamdu shaka ofisini
kwake alipotakiwa kueleza shutuma zilizotolewa na Dk Kijo Bisimba
alipohojiwa na shirika la habari la BBC akidai serikali inabana upinzani
na kuuhesabu kama uadui pia kuminya uhuru wa habari.
Shaka
alisema kwa kumuamini mwanaharakati huyo kama msomi mwenye upeo,
mchambuzi hodari na mtetezi wa masuala ya kisheria, haikutegemewa
ayafumbie macho matamshi ya Mbowe na kuishutumu kinafiki serikali ya
Rais Dk john Magufuli na kuongopa inadumaza demokrasia nchini.
Alisema
kama kuna kipindi ambacho serikali imekuja na mpango mkakati wa
kuwaandaa wananchi kifikra ili kufanya kazi na kuachana na mazogo ya
siasa zisizo na tija ni katika awamu ya tano ambapo mikutano ya hadhara
inayopambwa na matusi na kukashfiana kusiko staha wala mipaka kutishwa
kwa maslahi mapana ya kulinda tundu za taifa.
"Mama
yetu nadhani sasa ameanza kuzeeka. Amepoteza uwezo wake mkubwa wa
kupambanua mambo kwa kutazama haki na usawa. Nasita kumwita mshabiki
badala ya kuwa mtumishi bora wa jamii pia nafikiri anazeeka vibaya
"Alisema Shaka.
Kaimu
huyo Katibu mkuu alisema imekuwa kawaida ya mwanaharakati huyo na kituo
chake kuisakama serikali kwa mambo ya kufikirika bila kukemea upande wa
upinzani pale unapofanya mambo hatarishi hasa ya kupoteza amani na
kuharibu usalama.
"Tunafahamu
fika kuwa Kituo chake cha sheria kimekuwa kikitumiwa vibaya na baadhi
ya wanasiasa kuendesha mikutano ya kiharakati , kishindikiza mapambano
dhidi ya serikali pia mara kadhaa kutaka kukivuruga chama
tawala.Tumewatambua na katu hatutawaonea aibu "Alisema Shaka
Hata
hivyo Shaka alimtaka Dk Kijo Bisimba kueleza kuwa uhuru mpana wa vyombo
vya habari uliopo nchini unapatikana sehemu gani katika bara la Afrika
hata afikie kutamka kuwa uhuru wa watu kujieleza Tanzania umepotea.
Alisema
ikiwa mwanaharakati huyo anahitaji uwepo uhuru holela wa habari,
mikutano ya ovyo ya kisiasa , demokrasia isio na adabu na watu
kutofanyakazI za uzalishaji mali viwandani na mashambani akitaka waachwe
waogee porojo vijiweni, wakati huo umepita na hautarejea tena.
"Dk
Kijo Bisimba atueleze kina nani na vyama vyao hivi sasa wanandamana
baada ya chaguzi kuu aidha ufaransa, ubeligiji, Marekani, uingereza au
nchi za scandnavia .Tanzania nayo ni nchi huru yenye sheria na katiba
yake .Watu watii sheria na maagizo ya serikali "Alisema
Hata
hivyo Shaka aliitaka serikali ya Rais Dk Magufuli kuendelea na mipango
ya kuwatumikia wananchi na kusema wote wanaoishitumu serikali kwa
shutuma za kupika na kutaka kuikwamisha ndio watakaokuwa wa kwanza
kushangilia mafanikio ya kiuchumi na kihuduma pale yatakapodhihirika.
"Demokrasia
isio na heshima wala mipaka hatutaki iyagharimu maisha ya wengine. Wapo
watu wako tayari kuona mambo yakiharibika wakimbilie nje kusaka hadhi
za ukimbizi ili waishi ughaibuni tunaishauri serikali kuendelea kulinda
na kusimamia haki na sheria kwa kadri katiba yetu inavyoelekeza".
Alisema
0 Maoni