Unordered List


ANZISHENI KAMPENI ZA KUHAMASISHA UPIMAJI WA VVU-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
.............................................

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini washirikiane na wadau wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema.

Kadhalika, amewaagiza Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kwa kusaidiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wasimamie kwa uzito unaostahili kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo(Jumanne, Juni 19, 2018) wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema, iliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri, jijini Dodoma.

“Kwa vile tunazindua kampeni ya kupima na kuanza ARV mara moja (Test and Treat) natoa rai kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosheleza katika kila kituo kinachotoa huduma katika kila Mkoa na Wilaya,” amesema. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizo ya VVU waelewe kuwa utaratibu wa sasa ni kuanza dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha kinga mwilini, yaani CD4.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea tuzo ya kutambua kukubali kuwa Balozi wa kuhamasisha wanaume kupima VVU nchini, kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Flora Kamwela, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU  na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihamasisha upimaji wa Virusi vya  Ukimwi hususani kwa wanaume, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na kapteni Geofrey Mwajombe katika Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, katikati ni Sajenti Deogratius Peter.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akihamasisha pimaji wa VVU hususan kwa wanaume, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter. 

Chapisha Maoni

0 Maoni